Blessed Tajiri
JF-Expert Member
- Dec 16, 2023
- 284
- 870
Abiria wa ndege ya Precision Air kutoka Mwanza kwenda Dar es Salaam safari yetu ilikuwa leo Jumamosi April 11, 2026 saa saba mchana lakini mpaka sasa hatujui safari itakuwa muda gani!
Tumefika airport wanatuambia hakuna ndege, na hawatupi sababu za kwanini hakuna ndege au labda kusema pengine kutakuwa na delay ya muda fulani. Tumetafutiwa hoteli lakini mpaka wakati huu saa kumi na moja hii hatuelewi tutaondoka saa ngapi au lini na watu tuna ratiba na majukumu yetu.
Au mpaka atokee Zungu mwingine afanye vurugu ndio tuelezwe sababu ya hii changamoto? Kwani hata kama kuna hitilafu au hali ya hewa ni mbaya mnashindwa kutuambia nini walau tuelewe situation ilivyo na kupangilia mambo yetu vizuri kulingana na changamoto hii?
Pia soma: KERO - Precision Air mnatukosea sana Abiria, tangu Saa 12 Asubuhi Dar-Arusha tumeshindwa kuondoka kwa wakati na hamtoi maelezo
=====
UPDATE
Asanteni sana JF kwa kutusemea kwenye mitandao. Tumeambiwa tutaondoka leo na ndege ya saa kumi jioni, lakini mpaka sasa hatujaelewa delay hiyo imesababishwa na nini!
Pia soma ~ Precision Air, acheni masihara na maisha ya watu, abiria tumetumia Saa 24 kusubiri kuendelea na safari hapa Kilimanjaro Airport