Hivi mnaamini kabisa nauli yaweza kuwa 32,000/-?
Mimi yangu macho, nasubiri kusoma hapa comments zenu za kulaumu na kulaani!
Precissionair FOREVER! Mimi ni abiria tu msininange tafadhali!
Usiogope watu kukunanga, observation yako nzuri na kwa wale wanaotumia usafiri wa ndege hata kama ni mara tatu kwa mwaka watakuunga mkono, nauli ni kweli 32,000 lakini kwa watz wengi ambao safari zao si za mpangilio bado amabapo mtu anapanga safari wiki moja kabla hawezi kupata hiyo huduma, ili uweze kupata inabidi upange safari yangu 2 weeks ni advance na kwa mwezi wa December mpaka tarehe 28 na mpaka January 10 nauli inacheza 80,000, 96,000 na 112,000 ikiwa utafanya booking ili uondoke tarehe 6 (nimepitia wensite yao), kwahiyo ukiangalia kwa haraka haraka go and return kipindi hiki ni kati ya 160,000 na 214,000. Kwa wale wadharula mfano kama unataka kuondoka kesho au keshokutwa nauli ni kati ya 144,000 na 160,000 (oneway) kurudi inategemea lini kama utarudi baada ya wiki maana yake utalipa 96,000, 112,000 au 80,000 inategemea na muda utaoondoka hivyo assuming utalipa 112,000 maana yake utalipa 272,000(return).
Hivyo mdau observation yako ni nzuri ila kwa wale wanaojipanga mfano kama unataka kuondoka kuanzia January 18 ticket unapata maana na hawa jamaa ni wajanja si unajua huu ni mwezi wa masikukuu na wao wamepandisha kidogo
Back to uzi, bado precisiom air ataendelea kutamba tu maana nauli mpaka jana ilikuwa 208,000 (return) kwa wale wazee wa unaondoka keshokutwa booking unafanya leo na hao ndio wengi mdau maana kwa fast jet mfano ukitaka kuondoka kesho nauli ni 160,000 si unaona gap hilo
Na ndio maana precision air nae ameshituka karibu kila siku anapeleka mwanza boeing maana wengi hupenda kusafiri saa 1 na robo amefika sio anakaa masaa 2 na ATR