Precission air Hoi! KQ yahusishwa.

Mzito Kabwela

JF-Expert Member
Joined
Nov 28, 2009
Posts
18,887
Reaction score
7,673
Hali ya shirika la ndege la Precission la Tanzania inaelezwa kuwa 'mbaya' huku shirika la ndege la Kenya(KQ) likihusishwa na matatizo ya sasa ya shirika hilo.

Tayari Precission imeanza kufunga baadhi ya ofisi zake zilizopo nje ya nchi huku ikirudisha baadhi ya ndege zake aina ya Boing ilizokodi kwa ajili ya kuongeza maeneo inakofanyia safari zake.

Raia Mwema limeambiwa kwamba kuna hofu ya ukweli kwamba shirika hilo linaweza kutangaza kupunguza wafanyakazi wake wakati wowote kuanzia Leo.

Miji ambayo tayari Precision imefunga shughuli zake ni Lusaka Lubumbashi na Kinshasa.

Uongozi mbovu wa aliyekuwa Mtendaji Mkuu wa shirika hilo Alfonce Kioko, raia wa Kenya na kutofanya vizuri kwa shirika hilo wakati wa zoezi lake la kutaka kuuza hisa kwenye soko la Hisa la Dar es salaam ni mambo mawili makubwa yaliyochangia hali ya Precision kwa sasa.

Raia Mwema limepewa tuhuma mbalimbali za kifisadi kumhusu Kioko lakini inazihifadhi kwa ajili ya kuzifanyia uchunguzi zaidi badae.

Kioko alikuwa ni Pendekezo la KQ kuongoza Precision ingawa utendaji wake ulionyesha matatizo tangu awali, mwanzilishi na mwenyekiti wa Precision, Michael Shirima alikuwa akimkingia kifua.

Shirima ndiye mwenye hisa nyingi 35% huku KQ ikiwa na 34%.

Wadadisi katika sekta ya Anga nchini wanadai kwamba matatizo haya ya Precision yana mkono wa KQ ambayo inataka kutawala eneo la Afrika mashariki.

Sababu zilizotolewa ni mosi Kioko alikuwa Chaguo lao, Pili kushindwa kwa Precision kupata faida kwenye IPO kulichangiwa na kutopata wateja wengi Kenya na tatu ni hatua ya KQ kuanzisha safari za shirika hilo kati ya Nairobi na Kilimanjaro katika kipindi hiki cha matatizo ya Precision.

Wakati wa IPO, Precision ilitaraji Wakenya na Watanzania wengi wangeshiriki, cha ajabu Mamlaka za Kenya zikachelewesha uuzwaji wa hisa Kenya na waliporuhusu ikawa imechelewa.
 
na bado

watanzania tutalala wee.....tukiamka kila kitu tumewaachia wageni hasa wakenya

inaelekea woote tumesahau jinsi ile jumuiya ya kwanza ya afrika mashariki ilivyovunjika 1977

elimu elimu elimu ni muhimu sana
 
Ukijiunga na Wakenya ni kujimaliza tu.
Kumbuka mwekezaji mmoja kutoka kenya alivyoua General tyre ili auze YANA tyre si watu wazuri wale
 

Mkuu hata hiyo KQ yenyewe haiko salama sana kwa sasa. Naona yule nguli wa uongozi wa makampuni nchini Kenya bw. Titus Naikuni amefika ukomo.

Mimi nilishangaa sana IPO ya Precision kufanya vibaya nikabaki kujiuliza kwamba a promising company kama Precision kwa nini ifanye vibaya kwenye IPO kumbe jamaa wa nchi jirani walikuwa wakihujumu! Hawa jamaa hatari kwelikweli tuwaangalie kwa umakini wasije wakaimaliza Serengeti yetu (bia).
 
...wajiunge na fast jet ili wamshinde mkenya...nyasi ndo zitaumia..baada ya ushindi watengane wawe ka walivyo sasa...
 
Hii precision ni kampuni binafsi......lakini kuhusu hujuma za nchi jirani za kwa biashara za Tanzania, hapo ndio tunaona kuwa na TISS inayowajibika kwa maslahi ya nchi badala ya watu..... precosion ina semekana ni yakina mramba, TISS mko wapi? tena iliwahi kupewa Government Guarantee na kuweza kukopa ulaya......haya kuna suala la General Tyre Ltd, ni yale yale, sasa waweztu TISS wanafanya nini?

 
na bado

watanzania tutalala wee.....tukiamka kila kitu tumewaachia wageni hasa wakenya

inaelekea woote tumesahau jinsi ile jumuiya ya kwanza ya afrika mashariki ilivyovunjika 1977

elimu elimu elimu ni muhimu sana

Kwani umesahau kuwa zile sababu za kuvunjika jumuiya zilikuwa kwa ajili ya kufaulu mtihani tu?
 
mchaga na ujanga wako wote unaingia mchakato la wakenya, wakenya ni frndz 4 benefits
 

Mkuu get your facts straight. Dont get it all mixed up.
Mramba hana uhusiano wowote na Precision Air. Michael Shirima ambaye ndo muasisi wa hilo shirika akiwa na asilimia 35 ya shares kwa sasa, watoto wao wameoana. Mtoto wa Shirima na mtoto wa Mramba. Kwa hiyo wale ni wakwe tu.
Tatizo watu wakionekana wawili wanaanza ku associate vitu visivyokuwepo na kuvifanya vipo.
We ukimtembelea mkweo kwani ni lazima uwe una biashara nae?
Get the facts.
Na precision kwa sasa sio private company tena. Its a PLC. Find out more the difference between private limited companies and PLC.
 
Hivi hili Shirika si ndio kuna Mbunge alikuwa anapiga porojo bungeni libebeshwe jukumu la kuwakilisha nchi kama Shirika la Ndege la Kitaifa...
 
Wakenys si watu wa kupiga collabo nao bila kuweka walakini
 
Huu ni uongo na upuuzi wa watanzania kila wanapokuwa na matatizo wanajaribu kuwasingizia watu wengine. Mwandishi wa Raia Mwema umekaa ofisini kwa Dar unaandika habari za kimajungu majungu. Hata huko Kenya KQ ina hali mbaya ya kifedha kwa sasa, inakuwaje iiue Precision Air ambako wana hisa na ijiue yenyewe?? Acheni hizo tabia zenu, Lazy but knows it all atitude haitawasaidia waandishi wa habari wa Tanzania.

Mimi Ulukolokwitanga ni mteja wa PW kwa miaka mitano sasa, at least kila mwezi nawachangia hawa jamaa. Kwa maoni yangu kama abiria PW hii ya Sauda Rajabu imechoka sana ukilinganisha na ile ya Alfonse Kioko. Hii ya saizi haina hata ratiba ya ndege, kila siku kuna zaidi ya nusu ya ndege za PW zinachelewa kuondoka. Yes hata wakati wa Kioko kulikuwa na delays, lakini sasa ni mara 25 zaidi. Enzi za Kioko wafanyakazi walikuwa nidhamu na heshima kwa wateja, saizi hakuna nidhamu tena. Huyu mama ameondoa hadi BIA kwenye ndege na huku bei ya ticket ikipaa mara dufu, enzi za Kioko tulikuwa tunapata hadi offa ya bei, kwa sasa imebaki historia. Yes huenda jamaa alikuwa na mapungufu kama binadamu lakini sio kwa vile ni Mkenya, hili andiko ni la kibaguzi lenye lengo la kuficha udhaifu wa huyu dada wa Kiswahili kwa kisingizio cha matatizo nimeyakuta, kama matatizo umeyakuta so what? We si ndio CEO, tatua hayo matatizo kwa skills zako sio kupita magazetini kusema matatizo kayaleta mtangulizi wangu. Huu upuuzi watanzania tusiukubali kabisa, mtu kaomba kazi akijua kuna changamoto, anashindwa kuzitatua anasingizia mtangulizi wake, bull shit. Kama umeshindwa kazi Sauda achia ngazi.
 
Why the hell discussing private entities in names of Nationality???!!!!!!
 


kaka mbona unakua mkali una hisa nini?
Nimeongea na mtu wa precision aliniambia kuna baadhi ya strategic decisons ambazo zilikua wrong ndio zimewafikisha hapa.Kwa hiyo kinachofanyika sasa ni kuwithdraw baadhi ya routes ambazo zinaligharimu shirika ,then kubaki na ATR's ambazo ni cost effective kwa muda,then baadae hali itakapotulia ndio warejeshe na boeing.Mimi kwa mtizamo wangu , huu ulikua ni mpango kabambe wa kuhamisha fedha zetu, kwenda nje,na hivyo kuanzisha shirika jingine.Kwa hasara aliyosababisha Kioko haiwezekani kueleweka katika hali ya kawaida.

unles hilo shirika lilikua linaendeshwa kifamilia zaidi kwa kuaminiana kama ndugu.
 
I knew it was coming, tangu mwanzo i was one of those guys who were totally against the strategic alliance btn KQ an PA. I knew it was not a WIN WIN alliance but only a WIN LOSE business alliance. Nilipoona baadhi ya board of directors members wa PA ni members wa KQ nkajua hii shirika limekwisha.

Nchi yangu TZ inaangamia kwa kukosa maarifa!
 
Toka lini mswahili akawa mfanyabiashara sembuse CEO? Walichemka.
 

Managers always make bad decisions, haina ubishi. Mfano safari ya Lumbumbashi na Lusaka zilikuwa hazilipi, lakini ilikuwa ni strategy nzuri kwa shirika ku expand. Hata kama ungekuwa wewe, shirika halina ushindani wa ndani na umelikamata soko lote la ndani, then unatakuwa kufanya expansion, ungeenda nchi gani? Trip zenye hela katika soko la Tanzania ni Dar - Nairobi, Dar - Mwanza na Dar - KIA, ukizishika hizo unaexpand. Kama unajua kidogo corporate management huwezi kusema KQ wametorosha hela, hayo ni maneno ya mtaani. Hata huko kwa Kenya wana struggle kwa sasa.

Na huyo aliyekuja na strategy ya kutumia ATR ndio analiua shirika. Mimi nataka kwenda KIA napanda FASTJET ambayo inatumia muda mfupi na bei nafuu, siwezi kupanda PW, hivyo hivyo kwa Mwanza kwa vile ATR inatumia dakika 40 zaidi hewani na kwa vile inabeba abiria wachache ina maana kuwa bei yake ni kubwa. First year student wa Strategic Management anaweza kuelewa hilo.

Ngoja tuone huyo Sauda Rajabu atafanya nini, lakini hii tabia ya watanzania kuficha failures migongoni mwa watu eti Precision ni ya wakenya wanaiua na huku hela zao zimo ndani, nonsense.
 
Ukisikia watanzania kwa kulalamika ndo hapa, Precision inaajiri kindugu weeeeee halafu leo inasingizia wakenya,
Nasikia huko Precision kuna mtu haeleweki kaletwa kufanya nini kazi yake kuwakoromea wenzie kisa kampuni ya dada!
Na bado mtakoma!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…