Mzito Kabwela
JF-Expert Member
- Nov 28, 2009
- 18,887
- 7,673
Hali ya shirika la ndege la Precission la Tanzania inaelezwa kuwa 'mbaya' huku shirika la ndege la Kenya(KQ) likihusishwa na matatizo ya sasa ya shirika hilo.
Tayari Precission imeanza kufunga baadhi ya ofisi zake zilizopo nje ya nchi huku ikirudisha baadhi ya ndege zake aina ya Boing ilizokodi kwa ajili ya kuongeza maeneo inakofanyia safari zake.
Raia Mwema limeambiwa kwamba kuna hofu ya ukweli kwamba shirika hilo linaweza kutangaza kupunguza wafanyakazi wake wakati wowote kuanzia Leo.
Miji ambayo tayari Precision imefunga shughuli zake ni Lusaka Lubumbashi na Kinshasa.
Uongozi mbovu wa aliyekuwa Mtendaji Mkuu wa shirika hilo Alfonce Kioko, raia wa Kenya na kutofanya vizuri kwa shirika hilo wakati wa zoezi lake la kutaka kuuza hisa kwenye soko la Hisa la Dar es salaam ni mambo mawili makubwa yaliyochangia hali ya Precision kwa sasa.
Raia Mwema limepewa tuhuma mbalimbali za kifisadi kumhusu Kioko lakini inazihifadhi kwa ajili ya kuzifanyia uchunguzi zaidi badae.
Kioko alikuwa ni Pendekezo la KQ kuongoza Precision ingawa utendaji wake ulionyesha matatizo tangu awali, mwanzilishi na mwenyekiti wa Precision, Michael Shirima alikuwa akimkingia kifua.
Shirima ndiye mwenye hisa nyingi 35% huku KQ ikiwa na 34%.
Wadadisi katika sekta ya Anga nchini wanadai kwamba matatizo haya ya Precision yana mkono wa KQ ambayo inataka kutawala eneo la Afrika mashariki.
Sababu zilizotolewa ni mosi Kioko alikuwa Chaguo lao, Pili kushindwa kwa Precision kupata faida kwenye IPO kulichangiwa na kutopata wateja wengi Kenya na tatu ni hatua ya KQ kuanzisha safari za shirika hilo kati ya Nairobi na Kilimanjaro katika kipindi hiki cha matatizo ya Precision.
Wakati wa IPO, Precision ilitaraji Wakenya na Watanzania wengi wangeshiriki, cha ajabu Mamlaka za Kenya zikachelewesha uuzwaji wa hisa Kenya na waliporuhusu ikawa imechelewa.