Pregnant na Tumbo linajaa gesi!

Pregnant na Tumbo linajaa gesi!

condorezaraisi

JF-Expert Member
Joined
Sep 4, 2011
Posts
225
Reaction score
116
Mdogo wangu ni mjamzito 5 month ila kila siku analalamika tumbo linajaa gesi na anaweza kukaa week au na nusu hapati choo.
Anakula vizuri bila shida ila hizo gesi ndio zinamsumbua na choo ,Naomba msaada tumsaidieje?
 
Mdogo wangu ni mjamzito 5 month ila kila siku analalamika tumbo linajaa gesi na anaweza kukaa week au na nusu hapati choo.
Anakula vizuri bila shida ila hizo gesi ndio zinamsumbua na choo ,Naomba msaada tumsaidieje?

Ale ndizi tatu kwa siku za kuiva na maziwa mtindi ili kutoa gesi niliambiwa na dr wangu
 
Mdogo wangu ni mjamzito 5 month ila kila siku analalamika tumbo linajaa gesi na anaweza kukaa week au na nusu hapati choo.
Anakula vizuri bila shida ila hizo gesi ndio zinamsumbua na choo ,Naomba msaada tumsaidieje?
condorezaraisi, pole sana... Tumbo kujaa gesi hutokea mara nyingi kwa wajawazito kwani kichocheo kiitwacho progesterone ndio kinakuwepo wakati wa ujauzito na hiki hufanya mfumo wa uyeyushaji wa chakula kupungua, hivyo kukosa choo na wakati mwingine tumbo kujaa gesi..., pia tumbo linapozidi kukua hali hii inaweza kuongezeka hivyo nakusahuri, anywe maji ya kutosha na kula matunda kama maembe na ndizi kusaidia kupata choo. kuhusu gas anaweza kutumia antacid kama mucogel, au ya vidonge haina madhara kwa mjamzito.
 
Last edited by a moderator:
Namshauri ale chakula on time, asichelewe wala asipitilize mda wa kula. Mm nilikuwa ivyoiyvo lakini ilikuwa nikipitiliza kula au nikichelewa. Pia asiwe anavumilia sana hewa chafu 'ushuzi' ikija ajitahid kwenda kuitoa. Ni ayo tu!
 
Pamoja na ushauri Wa waliotangulia hapo, pia ngoja nikuitie na huyu daktari Wa JF:
MziziMkavu where are you doc'!
 
Last edited by a moderator:
Mkuu.@condorezarais Mpe Pole mdogo wako mwambie abadilishe vyakula ana matatizo ya ukosefu wa kutopata choo kiurahisi tizama hapa.


  • MARADHI YA KUTOPATA CHOO (CONSTIPATION): Haya ni maradhi ambayo mgonjwa huwa hapati choo kwa wepesi. Haja kubwa inaweza kutoka baada ya siku moja au mbili au zaidi na ikitoka huwa ni kigumu na hutoka kwa shida na wakati mwingine huwa kama

    cha mbuzi. Wagonjwa wengine hupata maumivu wakati wa kwenda haja kubwa.
    Mtu mwenye afya nzuri hupata haja kubwa kwa kiwango cha chini mara moja kwa siku. Na choo huwa laini na hutoka bila matatizo.

    SABABU ZA MARADHI HUSIKA:
    (1) Upungufu wa vitamini mwilini hasa vitamin B. (2) Maradhi ndani ya utumbo mpana. (3) Kula vitu vigumu na vikavu kama vile vyakula vya ngano. (4) Upungufu wa ulaji matunda na mboga. (5) Kutokunywa maji ya kutosha. (6) Upungufu wa fibre kwenye chakula zinazopatikana kwenye maganda ya mahindi. (7) Ukosefu wa kufanya mazoezi ya viungo.

    TIBA: Kanuni ya kwanza:

    Chukua glasi moja ya maziwa freshi baridi uchanganye na vijiko viwili vikubwa vya asali na kijiko kimoja kidogo cha mafuta ya habitsoda. Kunywa glasi moja kutwa mara mbili asubuhi na jioni. Dawa hii hufanya choo kuwa laini na kupata haja kubwa kwa wepesi.

    Kanuni ya pili: Unga wa sanamaki kijiko kimoja kikubwa, Unga wa tangawizi kijiko kimoja kikubwa, Unga wa habasoda kijiko kimoja kikubwa, na Asali robo lita. Dawa hizi zote zichanganye pamoja kwa kukoroga kwa kijiko. Kula kijiko kimoja kutwa mara tatu.

    Kanuni ya tatu: Asali robo lita, na Unga wa Arki susi vijiko vinne vikubwa. Kula vijiko viwili vikubwa kutwa mara mbili.

    Kanuni ya nne: Kunywa kwa wingi maji ya kunywa ya kutosha na pia ule kwa wingi matunda na mboga.


    Kanuni ya tano: Kula kila siku asubuhi tende saba kabla ya chakula cha asubuhi. Tende hufanya choo kuwa laini. Mkuu.@condorezarais tumia Dawa zangu kisha unipe feedback.


  • UKOSEFU WA CHOO: Soma tiba rahisi



    UKOSEFU wa choo ni tatizo sugu miongoni mwa watu wengi. Bila kujua kuwa ni tatizo ambalo linahitaji tiba

    ya haraka, watu wengi hupuuzia na kuona siyo tatizo kubwa na ni hali ya kawaida. Ukosefu wa choo wa

    muda mrefu, huwa ndiyo chanzo cha magonjwa mengine hatari.

    Mtu anapokosa choo kikubwa kwa siku kadhaa, uchafu hujikusanya tumboni na unapokosa sehemu ya kutokea

    hukimbilia kwenye damu na kuingia kwenye mfumo mzima wa damu. Uchafu huo unapoingia kwenye

    mfumo wa damu huwa sumu na chanzo cha maradhi mengine ambayo hujitokeza baadae na kuanza kumuathiri mtu, bila kujua chanzo chake.

    Kwa kawaida mtu unapaswa kupata choo cha uhakika japo mara moja kwa siku, kutegemeana na mlo wake

    wa kila siku, unapokosa choo kwa siku nzima ili hali una kula milo yote kwa siku, elewa una tatizo katika

    mfumo wako wa kusaga chakula hivyo unapaswa kuchukua hatua haraka.

    MTU MWENYE TATIZO HILI ANA DALILI GANI?

    Mtu mwenye tatizo la ukosefu wa choo huwa na dalili kadhaa, ikiwemo kutumia nguvu na muda mwingi wakati wa kujisadia haja kubwa. Pili ulimi wake huwa

    na utandu mweupe na hutoa harufu mbaya mdomoni. Mtu huyu pia hukosa hamu ya chakula na wakati wote tumbo huwa limejaa.

    NINI HUSABABISHA TATIZO?


    Tatizo la ukosefu wa choo husababishwa zaidi na ulaji mbaya wa vyakula, kuacha kula matunda na mboga na

    staili mbaya ya maisha ikiwa ni pamoja na kutokunywa maji ya kutosha kwa siku.

    NINI KIFANYIKE?

    Ili kuondoa tatizo kabla halijawa sugu, fanya moja miongoni mwa haya yafuatayo: Kunywa maji ya

    uvuguvugu asubuhi mapema, kisha tembea tembea, baada ya muda utasikia haja ya kwenda chooni. Ili

    usifanye haraka na upate muda wa kutosha kujiandaa kwenda kazini, amka mapema zaidi. Kula kiasi cha

    kutosha cha salad ya mboga mboga na juisi ya matunda halisi asubuhi kabla ya kula chochote.

    Kila siku kabla ya kwenda kulala, kunywa maji ya uvugu yaliyochanganywa na kijiko kimoja cha asali. Kunywa maji ya uvugu

    yaliyochanganywa na limau asubuhi na mapema kabla hujala kitu chochote. Kunywa ‘castor Oil’ muda mfupi kabla ya kwenda kulala. Ili

    kujiepusha kabisa na tatizo la ukosefu wa choo, jenga mazoea ya kunywa maji mengi, kula mboga na matunda kwa wingi kila siku na

    kuacha kabisa ulaji wa vyakula vilivyoondolewa virutubisho kama vile mikate myeupe, ugali wa unga mweupe, keki vyakula vyenye sukari nyingi na vyakula vingine vitamu.

 
Mdogo wangu ni mjamzito 5 month ila kila siku analalamika tumbo linajaa gesi na anaweza kukaa week au na nusu hapati choo.
Anakula vizuri bila shida ila hizo gesi ndio zinamsumbua na choo ,Naomba msaada tumsaidieje?

Vp kujamba jamba? Anajamba kwa sauti au kimya kimya na vipi ushuzi wake unanuka sana?
 
pole ni jambo la kawaida inasababishwa na kuongezeka progestrone mwilini ambayo hupunguza peristalisis za tumbo na kusababisha indigestion.
Pili kwa watu wanaotumia iron sulphate, husababisha indigestion na constipation pia.
Dawa hakuna labda iwe very severe sana kama more vomitting na kusababisha IO or intestinal obstraction. Ndo utaitaji matibabu ya hospital.
Kama ni FeSO4 jaribu kuacha then usupliment na nutrition za kuongeza iron
 
Kuna watu wamesema vyema hapo juu, mimi ni mgeni lakini nimeguswa na tatizo la dada yetu.

Ni kweli kwamba kukosa choo (coinstipation) na tumbo kujaa gas (dyspepsia and ) ni matatizo ya kawaida kwa wajawazito.

Ni kweli pia kama walivyoeleza wengine kwamba hii kwa kiasi kikubwa husababishwa na kichocheo kiitwacho 'progesterone' ambacho huzalishwa kwa wingi mama anapokuwa mja mzito. Kazi ya kichocheo hiki ni kulifanya tumbo la uzazi (uterus) li-relax ili mimba isitoke (kinazuia uterine contractions).

Lakini zaidi ya effect yake kwenye tumbo la uzazi, pia hufanya relaxation ya misuli mingine mwilini hasa ile misuli laini (smooth muscles). Kati ya misuli inayoathiriwa na kichocheo hiki ni ile ya utumbo na ya mlango (cardiac sphincter) unaotenganisha tumbo na njia ya juu ya kupitisha chakula (oesophagus).

Kinachotokea utumbo uki-relax unasababisha kudorora kwa utembeaji wa utumbo (bowel movements) na hivyo kusababisha yale mabaki ya chakula ambayo yamegeuzwa kuwa uchafu (feaces) yachelewe kutolewa nje ya mwili. Hivyo mtu anaweza kuchelewa kupata choo na hivyo anakuwa coinstipated.

Ile sehemu ya mlango nayo (cardiac sphincter) iki-relax kutokana na effect ya progesterone, gas iliyoko tumboni hupanda juu kwenye oesophagus (anapata kama aina fulani ya gatro-eosophageal reflux) na kusababisha kiungulia (heartburn).

Matibabu

Kwa coistipation ajitahidi kuwa active kwa kufanya mazoezi kama kutembea, kuogelea nk., anywe maji mengi, atumie matunda ya kutosha kama mapapai, hata maparachichi na mboga mboga pia. Iron supplements pia zinaweza kusababisha coinstipation hivyo muone daktari wako ajue namna ya kukusaidia kama kukupa dawa ambazo zina kiasi kidogo cha iron.

Kwa heartburn na dyspepsia anaweza
1) Kufanya marekebisho kwenye mfumo wake wa maisha (life-style modification) kama
a) kula chakula kidogo kidogo mara nyingi, sio kingi kwa wakati mmoja,
b) asile chakula usiku sana, akichelewa mwisho saa 2.,
c) atumie mto wakati wa kulala ikiwezekana kitanda kinyanyuliwe kichwani kuzuia gas isipande juu.
d) Atumie chewing gums zinasaidia kupunguza acid,
e) aepuke vyakula vinavyoongeza uzalishaji wa acid kama maharage, pilipili na spicy foods nyingine.

2) kutumia dawa zinazopunguza acid au uzalishaji wake kama
a) cimetidine na ranitidine ambazo hazina matatizo pia kwenye ujauzito na hazileti coinstipation
b) Magnesium trisilicate ambayo pia ni salama kwa mama mjamzito ingawa dawa hii inaweza kusababisha coinstipation. Isitumiwe kwa zaidi ya wiki. Muone daktari bingwa wa akina mama in-case tatizo litaendelea.

Asitumie dawa iitwayo Omeprazole (ingawa hutumiwa pia kupunguza acid kwa wasio wajawazito) kwani imeonyesha kuleta madhara kwa mtoto hata kifo kwenye utafiti uliofanywa kwa wanyama.

Matatizo yakizidi muone specialist wako.
 
Yaani MziziMkavu ..unga wa Arki ndo unga gani maana utatusaidia wengi
Unga wa Arki susi unapatikana kwenye maduk ya madawa ya kisuna ni mti unautwanga unageuka unga nenda kaulize kwenye maduka ya dawa za kisuna utapata wanauza huo mti wa Arki Susi. Kwa Lugha ya kiingereza dawa hiyo inaitwa jina hili Liquorice angalia picha hapo chini dawa ya mti kabla ya kuwa unga halafu wewe mwenyewe unaitwanga kuwa unga.
 

Attachments

  • licorice_root_powdered__36706.jpg
    licorice_root_powdered__36706.jpg
    14.7 KB · Views: 605
  • Liquorice.jpg
    Liquorice.jpg
    20.9 KB · Views: 664
Back
Top Bottom