John Haramba
JF-Expert Member
- Feb 4, 2022
- 365
- 1,374
Mmiliki wa Klabu ya Chelsea, Roman Abramovich
Kumekuwa na presha kubwa kwa bilionea huyo kuiuza Chelsea kutokana na ukaribu wake na Rais wa Urusi, Vladimir Putin ambaye anasakamwa kwa kuamua jeshi la nchi yake kuanzisha mashambulizi dhidi ya Ukraine, hivi karibuni, jambo ambalo linasababisha iaminike kuwa anamuunga mkono Putin katika mgogoro huo.
Licha ya uongozi wa Chelsea kutosema kuwa kuna mipango ya kuuzwa kwa klabu hiyo lakini bilionea wa Marekani, Todd Boehly na Hansjorg Wyss wa Switzerland ni kati ya wanaotaka kutuma maombi wiki hii.
Abramovich,ameshatangaza kukabidhi majukumu yake ya utendaji kwa Bodi ya Udhamini ya Chelsea licha ya kuwa anaendelea kuwa mmiliki na inaelezwa kuwa ana mpango wa kuuza jumba lake la kifahari lililopo England.
Pia soma
1. Tajiri Roman Abromavich akabidhi timu ya Chelsea kwa Bodi ya Wadhamini wa club hiyo
2. Bodi ya Wadhamini Chelsea FC yasita kubeba mikoba ya bilionea Roman Abramovich
Source: The Sun