CHADEMA wakosa fedha za kurusha Live Mkutano wao na Waandishi wa Habari.
CHADEMA walitoa taarifa kuwa wangerusha moja kwa moja mkutano wao na waandishi wa Habari ambao ulipangwa kufanyika leo kuanzia saa tano Asubuhi. Taarifa zinasema kuwa chama hicho kilialika vyombo vya Habari vya Azam, ITV, Channel Ten na Radio kadhaa kurusha hewani mkutano huo.
Hata hivyo, mpaka leo saa mbili Asubuhi, CHADEMA wamekosa fedha za kurusha hewani Mkutano huo. Inaelezwa kuwa Freeman Mbowe amesema kuwa chama hakina fedha kwa vile walitumia fedha nyingi kugharamia Mkutano wa Kamati kuu kutokana na kuongezeka kwa siku za mkutano huo kutoka siku mbili zilizopangwa awali hadi siku nne. Naye kiongozi wa heshima wa CHADEMA, Edward Lowasa alipofuatwa kuokoa jahazi alijinu kuwa imekuwa ninghafla mno na kwamba wangemwambia mapema, angewasiliana na maswahiba wake wangemsaidia.
Ka hali hiyo, Mkutano huo umeshindikana kuwa Live na sasa rusubiri recorded au clips zilizoeditiwa.