Kati ya mzee JOSEPH BUTIKU na Dr. EMMANUEL NCHIMBI nani ana busara? (Hatima ya mkoa mkoa wa RUVUMA na viongozi wake
Kwa waliosahau, Dr. Nchimbi ndiye alikuwa mbunge wa Jimbo la Songea mjini 2010-2015.
Kwa waliosahau, Dr. Nchimbi ndiye alikuwa waziri wa mambo ya ndani wakati DAUDI MWANGOSI (Aliyekua Mwandishi wa habari wa Channel Ten) aliuawa na kundi la Polisi (mbele ya RPC wa Iringa wa wakati huo SACP KAMUHANDA) lililomzunguka na kumshambulia kwa kipigo kikali, Marungu na mateke hata alipodondoka chini waliendelea kumshambulia hatimaye walimpiga bomu la machozi tumboni wakamwaga utumbo wote palepale.
NB: Mpaka Leo hii, haijulikani kosa la marehemu DAUDI MWANGOSI lilikuwa ni lipi, au kwenye kamera yake alirekodi tukio gani hata Polisi wakachukia na kuamua kumshambulia kama mnyama.
Kwa waliosahau, Dr. Nchimbi ndiye alikuwa waziri wa mambo ya ndani wakati huo alilitetea jeshi la polisi kwa nguvu zote kwamba halina hatia na walikuwa katika kutekeleza majukumu yao ya msingi.
Kwa waliosahau, Dr. Nchimbi ndiye alikuwa waziri wa mambo ya ndani alimuhamisha RPC wa Iringa wa wakati huo SACP KAMUHANDA akampeleka makao makuu. Yaani hiyo kesi akaiamua yeye akahukumu Moja kwa Moja na akaona adhabu ya kumtosha SACP KAMUHANDA ni hiyo na askari wengine walioshiriki kumpiga mateke marehemu DAUDI MWANGOSI hawana hatia. Kama ambavyo SACP MALLYA aliposema "Binti wa Yombo alikuwa kama anajiuza" adhabu aliyopewa ni kuhamishiwa makao makuu.
Ikumbukwe katika press conference yake ya juzi ijumaa Dr. Nchimbi alisema sio sahihi kuvituhumu au kuhukumu moja kwa moja kuwa vyombo vya Dola vinahusika na matukio ya UTEKAJI na MAUAJI, wakati yeye alihukumu na akatoa hatima ya RPC KAMUHANDA.
Kwa waliosahau, Dr. Nchimbi ndiye alikuwa waziri wa mambo ya ndani wakati jeshi la polisi lilipomtoa kafara kijana mwenye umri wa takriban miaka 25 ndiye mwenye hatia ya kumuua DAUDI MWANGOSI.
Kesi ya bwana mdogo huyo iliendeshwa na wanaharakati na hatimaye akapatwa na hatia ya kuua bila ya kukusudia 😆😆😆😆
Kwa waliosahau, Dr. Nchimbi ni msomi wa masuala ya UJASUSI na USALAMA WA TAIFA na sehemu ya mafunzo hayo ameyapata nchini CUBA. Mtu wa namna hii ndiye Frontline kwenye SIASA za Tanzania kwa sasa akikabidhiwa kiti nyeti kabisa katika chama kama KATIBU MKUU. Jaribu kulinganisha makatibu wakuu wa CCM waliomtangulia kabla yake na yeye unaona nini kikitokea kwa CCM.
Kama yeye Dr. Nchimbi ni huyu CPA AMOSI MAKALA katibu mwenezi na Itikadi wa CCM. Zama za mwisho za AMOSI MAKALA kwenye siasa za ushindani AMOSI MAKALA alishindwa kwenye kura za maoni za ndani ya chama cha CCM, akaangukia kwenye ukuu wa mikoa Hadi alipopata nafasi hii.
Mtu kama Dr. Nchimbi hawezi kuwajibika wala kuwajibisha jeshi la polisi kwa namna yeyote ile. Rejea kifo Cha AQUELINA.
Kwenye press conference yake Dr. Alisema genge la watekaji linaloendesha matukio ya UTEKAJI na uuaji lina nia ovu ya kuligawa taifa na kuichonganisha serikali na wananchi wake na kujenga uhasama baina ya vyama vya SIASA. Akaenda mbali zaidi na kusema kwamba genge hilo la watekaji limepelekea hata baadhi ya watu wenye busara kuongea maneno yasiyo ya busara (miongoni mwao, naamini alimlenga mzee Joseph Butiku)
Kati ya mzee JOSEPH BUTIKU na Dr. EMMANUEL NCHIMBI nani ana hekima na busara??? Katika press conference yake mzee BUTIKU aliuliza waandishi wa habari "mnafikiri ni kwanini waziri Masauni alizomewa na wananchi na waombolezaji, nyie hamjui?"
Kwa waliosahau, Dr. Nchimbi ndiye alimpendekeza LEONIDAS GAMA kuachia ukuu wa mkoa wa KILIMANJARO kwenda kugombea ubunge wa Jimbo la Songea mjini kwenye uchaguzi mkuu wa 2015. Alifanya hivyo kwa sababu wana-SONGEA walimchoka, hakuna maendeleo aliyowaletea, aliwatelekeza, na alikuwa bize na nafasi mbalimbali za uwaziri alizoshika.
Kwa waliosahau, Dr. Nchimbi ndiye aliyeongoza WIZI wa kura za ubunge 2015 Jimbo la Songea mjini, ambapo LEONIDAS GAMA alishinda kwa kura 40,000 dhidi ya 38,000 za mgombea wa CHADEMA. Huku vurugu kubwa kati ya wananchi na Polisi zikishuhudiwa usiku kucha.
Kwa waliosahau, LEONIDAS GAMA hakumaliza kipindi chake alifariki Dunia kabla ya miaka mitano. Ilifanyika uchaguzi mdogo na CHADEMA walitangaza kususia uchaguzi huo kutokana na malalamiko na kasoro walizoainisha kwenye uchaguzi mkuu wa 2015 kutoshughulikiwa. Zaidi ya asilimia 50% ya Wananchi wapiga kura wa Jimbo la Songea mjini takriban 88,000 walisusia pia uchaguzi huo.
CCM walimchukua Dr. Damas Ndumbaro kutoka DSM alipokuwa anapiga kazi za deiwaka za uanasheria wa shughuli za mpira wa miguu, wakampeleka Songea kugombea ubunge akashinda kwa takriban kura 41,000 dhidi ya takriban kura 1,000 za mgombea wa ACT WAZALENDO.
Dr. Damas Ndumbaro naye anapita njia ya Dr. Nchimbi, baada ya kushinda ubunge anapewa nafasi mbalimbali za uwaziri anasahau Jimbo, hivi Sasa Yuko bize sana na maandalizi ya AFCON 2027 kesho kutwa atakuwa mgeni rasmi kwenye fainali ya CLAUDS Ndondo Cup RUVUMA.
Kwa mkoa wa RUVUMA, Ni mkoa uliojaaliwa kuwa na watu wanafanya kazi kwa bidii na kujituma kwenye nyanja zote kilimo, ufugaji, biashara n.k. lakini wamekosa viongozi wanaotamani kuhudumia wananchi. (Mtazame JENISTA MHAGAMA-mbunge wa Songea vijijini -Peramiho ndio makao makuu ya Jimbo) Yuko bize na serikali.
Songea kulikua na vyuo vikuu vitatu ambavyo vilichangia kuchechemua shughuli za kiuchumi na mwingiliano wa WATU, lakini vyote vilifungwa na kufutiwa leseni za usajili kwa sababu tofauti tofauti kila kimoja. Hakuna mbunge hata mmoja aliyewahi kuwafuata walikuwa wamiliki wa vyuo hivyo kujua kulikoni au tufanye nini ili mrejee.
Ndugu zangu, kwa msiopajua SONGEA, Songea ni miongoni mwa sehemu chache zilizobakia nchi hii ambapo unanunua kisado Cha mahindi kwa TShs. 500/= Hadi 1000/= au mgahawani unauziwa wali nyama TShs. 1000/=. Ukiwa na Tshs. Mil. 10/= unanunua kiwanja ekari 1 ndani ya SONGEA manispaa sio kijijini, unanunua tofali za kuchoma, unamlipa fundi, unainua nyumba ya vyumba 3, sebule, choo, stoo, jiko na master 1 ndani. Unaezeka ndio Mil. 10/= yako inaisha! 😀. Utatafuta pesa ya kufanyia finishing na kuvutia maji na umeme tu.
Kama ni mgeni umeshuka pale stand, Songea mjini Wana lodge za Hadi Tshs. 5000/= unaoga maji moto ila bafu lipo nje.
Mkazi mpya umehamia Songea kikazi kuna rooms kubwa za self-contained za Hadi Tshs. 25,000/= kwa mwezi 😀! Rooms za ukubwa huo huo ukienda MBEYA, IRINGA, MOROGORO, au DODOMA Zina bei ya kuanzia Tshs. 60,000/= Hadi 100,000/=
Mkoa wenye fursa kama hizo umekosa nini kupata maendeleo kama Si viongozi??
Na RUVUMA nzima kwa sasa ikifika kipindi cha uchaguzi mkuu, CCM wakitaka kupanga mikakati ya sera na ahadi za kwenda kunadi kwenye kampeni watamuuliza nani???? Kama sio Dr. Nchimbi, ndio mtu anaye tazamwa na CCM kama mwenyekiti wa viongozi wote wa RUVUMA, Unatarajia nini kitatokea kwa wananchi wa RUVUMA miaka 25 ijayo?
Kwa ufupi, wazururaji wa CCM wa sasa hivi ni watu waliopoteza mvuto kwa wananchi na Kisha wakakaliwa na wanachama wa CCM kwanza (rejea ADAM MALIMA) Kisha wakakateuliwa na chama kushika nyadhifa hizo za kuzurura au ukuu wa mkoa.