GE2025 Press Luhaga Mpina anazungumza na Wanahabari, leo Septemba 13, 2025

GE2025 Press Luhaga Mpina anazungumza na Wanahabari, leo Septemba 13, 2025

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

DogoWaNjombe

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
3,284
Reaction score
7,708
Mgombea Urais kupitia ACT Wazalendo, Luhaga Joelson Mpina, leo Septemba 13, 2025 anatarajiwa kuzungumza na Waandishi wa Habari baada ya kurejesha fomu zake katika Ofisi ya Tume Jijini Dar es Salaam.

Mkutano unafanyika Makao Makuu ya ACT Wazalendo – Magomeni.

Pia soma ~ ACT yakataa gari alilopewa Mpina na INEC
​


Dorothy Semu, Kiongozi wa ACT Wazalendo

Tunashukuru kwa ushindi tulioupata chama cha ACT Wazalendo kimeendelea kuwa Darasa la kudai na kupigania demokrasia Tanzania. Tulisema Tutashiriki tukipambana na tunapambana tukishiriki.

Imekuwa ni wiki mbili ngumu wiki mbili za ujasiri, za kujitoa, za kujiamini, kwamba mabadiliko ya taifa letu yataletwa na sisi wenyewe, kwamba chama cha ACT Wazalendo kimekuwa ni chama tumaini, tegemeo na kitakwenda kudhihirisha hivyo kwenye uchaguzi huu itakapofika Oktoba 29.

Hatuna shaka kwamba chama hiki kiliandaa wagombea makini, ambao wataenda kunadi ilani ya chama hiki, lakini pia wagombea watakaohakikisha tunaibuka washindi.

Tunashukuru viongozi wa chama ngazi zote kuanzia tawi, viongozi wa halmashauri kuu, kamati kuu, kamati ya uongozi na vitengo vingine vyote ambavyo vimeshiriki kikamilifu kuhakikisha hakikisha tunavuka jambo gumu lililokuwa mbele yetu. Haikuwa rahisi lakini tumeona ukomavu, uimara na uongozi wa chama.

Kampeni zilipoa, tumerudi na tumerudi imara.


Mgombea Mwenza ACT Wazalendo, Fatma Fereji

Tulipambana na tumeshinda, Mpina alikuwa anatupa moyo muda wote na kweli tumefanikiwa kushinda, leo siyo siku ya kuongea sana lakini tumelazimika kuja angalau kutoa neno.

Timu ya Mgombea Urais na Mgombea Mwenza zipo tayari kwa ajili ya kampeni ili kufanikisha Rais wa Jamhuri ya Muungano anatokea ACT Wazalendo. Sisi ni washindi.

Leo tunaanza rasmi kampeni, tutahakikisha tunawapatia Wananchi Viongozi Bora.


Luhaga Mpina, Mgombea wa urais kupitia ACT Wazalendo

Uteuzi kwa tume umekamilika, na sisi tunaishukuru tume kwa kutenda haki hiyo ambayo tayari uteuzi umekwisha fanyika na sasa safu ya vijana kutoka ACT Wazalendo imekamilika, kwa maana Rais wa Zanzibar, Othman Masoud Othman amekwishateuliwa na sasa anaendelea na kampeni.

Kama nilivyosema huku, kwa sababu ya nafasi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, nafasi ya makamu wa Rais zilipingwa na leo uteuzi umefanyika, walisema hatutakuwepo kwenye ballot paper, sasa tumekuwepo na kampeni zitaanza mara moja zikiwa zimepita siku 15. Wagombea wa ACT Wazalendo wamebakiwa na siku 45 kati ya siku 60 zilizotolewa kwaajili ya kampeni kwa wagombea wote.

Pamoja na hayo yote, nahodha mahiri hafundishwi kwenye maji yaliyotulia bali anafundishwa kwenye maji ya dhoruba na hivyo hizi siku 45 zinatutosha. Tutatembea kwenye majimbo yote, Tanzania bara na Zanzibar, Hata wagombea wetu wa nafasi za ubunge, udiwani msiwe na mashaka katika hilo tunakwenda kufanya kampeni mapema iwezekanavyo na tutaanza mara moja.


Sisi tupo tayari kwaajili ya kampeni, watanzania wote, wapenda mabadiliko wote ninajua huzuni na majonzi makubwa waliyonayo baada ya wagombea wao wa ACT Wazalendo kuzuiliwa kurejesha fomu, na ninajua furaha yao baada uteuzi kufanyika leo, na mimi nataka niwakikishie kwamba tumeomba hizi nafasi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tukiwa tayari na uzoefu wa kutosha, tunayajua matatizo ya watanzania, tukiwa tayari tuna uwezo wa kushughulika na matatizo ya watanzania, tukiwa tumekamilika kufanya kazi hiyo.

Suala la gari kama nilivyosema maelezo aliyoyatoa hapa Mwanasheria Mkuu ndio msimamo wa Chama chetu cha ACT wazalendo na ndio msimamo wa Mgombea Urais na Makamu wake kama, sisi chama na mgombea tunayo magari ya kutosha yanayotuwezesha kuzunguka nchi nzima kwenye kampeni kwa nini tulichukue hili gari la Watanzania ambalo linaweza likafanya kazi nyingine lakini la pili tulitaka ikawe 'hapa kazi tu'. Sasa kama tunataka ikawe kazi tu halafu tena huku na gari tena

Uchaguzi huu pamoja na kucheleweshwa kwa siku 15, tutashinda kwa asilimia 70, asilimia 30 watagawana mgombea wa CCM na na wale wengine na chama cha ACT Wazalendo kinaenda kuibuka kidedea katika uchaguzi huu wa mwaka 2025.

Suala la INEC kuiamini au kutokuiamini mimi ninachojua ni kwamba tume huru ya Uchaguzi itaenda kutangaza matokeo kama ambavyo yatakuwa yametoka ya kwamba wagombea wa ACT Wazalendo katika nafasi mbalimbali wameibuka kidedea.

Tume na mamlaka zote za umma zifanye kazi za umma, zifanye kazi kwa mujibu wa sheria, kama katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inavyowataka wafanye.

Vyama vya upinzani si wahaini na wala si wahalifu katika nchi yao, hivyo hakuna sababu yoyote ile ya kutumia mamlaka ya umma kuviadhibu vyama vya siasa

Vyombo vya Dola vitupe ulinzi tu, usitumie nguvu ya Dola kupata ushindi, kama Watanzania hawakutaki nenda nyumbani ukapumzike.

Vyombo vya Dola visitumike vibaya kwa kuwa unaweza kushiriki kufanya hujuma kisha ukashangaa Mpina anatangazwa mshindi, utaweka wapi sura yako.

Vyombo vya Dola vifanye kazi yao kisha viache mambo mengine yaamuliwe katika uzinduzi wa kura.

Mtajulishwa kuhusu ratiba ya Kampeni na michakato mingine.​
 
🚮🚮🚮🚮🚮 upuuzi mtupu ! Wenyenia njema wanahitaji reform! Ukiona kiongozi mwenye uelewa anashiriki mambo ya kipumbavu huku qkijuwa ni upumbavu mtupu ujue ana maslahi binafsi na swala hilo! Luhaga mpina na zitto kabwe hawa watu wawakatae watanzania kwa kusaliti watanzania wapenda mabadiliko
 
Back
Top Bottom