Presss ya Mawaziri leo, wanamaanisha nchi inajengwa na tozo tu?

Presss ya Mawaziri leo, wanamaanisha nchi inajengwa na tozo tu?

Hawa jamaa nimeamini wote wamepewa maelekezo ya kujibu kile alichozungumza Mbowe jana, mpaka Ndalichako nae amesema wanaangalia namna ya kupunguza machungu ya tozo kwenye mishahara ya wafanyakazi.

Ajabu, kama mtu mmoja anawaendesha hivi, siku watanzania tukiamka hawa jamaa ni wepesi sana, watapotea haraka sana kwenye ramani ya siasa za nchi hii.
 
Kwanza wamefanya press kwa kukurupuka tu. Hatujaelewa jambo lolote.

Pili, wamepunguza kodi ya madini toka 6% hadi 3%. Wakatutwisha mizigo hadi kwenye tumishahara ambato tusharipia kodi. Huu ni wizi na kukosa usimamizi wa rasilimali.

Kwa nini sasa tozo zinafanya kazi kubwa kuliko hata PAYE?. Kuliko hata kodi zingine zote?

Kwamba kabla ya tozo nchi ilikuwa haiendi?

Wanalamba asali na kutunyonya sisi tulioko chini?.

Rais mtoe kwanza huyu waziri wa fedha na mipango. Analeta siasa kwenye maisha yetu. Hayuko serious.

Anafabya kazi zake kivivu sana bila kutumia akili, ni kama kupiga bomi mortuary afu anajisifu kuwa na shabaha.


Kumbe Hata rudhuku ya mafuta mmehamihishia kwenye Tozo?

Kwanini lakini mnaishi maisha ya anasa huku wananchi wakilia?, Why? Mnatia hasira.
Kuna shida kwenye makuzi ya wengi wa vijana! wa sasa; watu tegemezi, wasio na uti wa mgongo!
Sioni vijana waliojisimamia tukapata uhuru. Sioni vijana aggressive.


Nimeshaandika hapa kuna kijana mmoja tu mwenye maono na mbunifu katika serikali hii. Hata uwaziri mkuu apewe wakati tunangojea kumkabidhi nchi.
Sijamsikia kwenye uchafu wowote, lakini madelu mara wakamatwe na wake za watu wa kampeni, mara uchawi kha.

HUSSEIN MOHAMED BASHE! Apewe uwazir mkuu haraka sana
 
Marehemu JPM angepandisha kodi na tozo zikawa juu hakuna hata mmoja wao angepiga kelele.

Miradi aliyoachiwa SSH ni mikubwa na inakula pesa nyingi. Kama mtu hataki tozo na asiwe wa kwanza kudai viwango katika ufanisi mzima wa serikali.

Huku ndiko kufunga mikanda kwenyewe.
Haya ndio madhara ya kuwachekea wapuuzi
 
Inasikitisha sana
Wale watu wanakula neema ya hii nchi usiombe

Niliwahi kuwa karibu na jamaa yangu mwenye kibarua huko karibu na hao jamaa aisee ni kufuru, huwezi kuamini hii nchi ni maskini kwa bata zile wanazokula waheshimiwa.

Kwanza wakipandishwa ndenge lazima iwe business class ukikata economy ujue litakukuta jambo baya
 
Kipindi cha JPM miradi kibao ilisonga mbele bila Tozo...
Mi nawakumbusha tuu kuwa mwezi huu walisema Treni ya Umeme inaanza kazi.

Na hata Juzi Tarura walisaini mikataba ya barabara za vijijini cha kushangaza bara bara yetu ya Ubena to Nger haija guswa na wala hawana mpango hadi hivi sasaaa
 
Nchi haiwezi kujengwa kwa tozo. Nchi inajengwa kwa kodi inayotokana na uzalishaji, jinsi uzalishaji unavyoongezeka ndiyo na kodi inaongezeka. Tozo kwa wananchi maskini kwenye shughuli ambazo siyo za uzalishaji ni kuendeleza umaskini. Unamtumia mtu kijijiji shilingi elfu tano eti anakatwa tozo kujenga nchi.
 
Back
Top Bottom