Presss ya Mawaziri leo, wanamaanisha nchi inajengwa na tozo tu?

Hawa jamaa nimeamini wote wamepewa maelekezo ya kujibu kile alichozungumza Mbowe jana, mpaka Ndalichako nae amesema wanaangalia namna ya kupunguza machungu ya tozo kwenye mishahara ya wafanyakazi.

Ajabu, kama mtu mmoja anawaendesha hivi, siku watanzania tukiamka hawa jamaa ni wepesi sana, watapotea haraka sana kwenye ramani ya siasa za nchi hii.
 
Kuna shida kwenye makuzi ya wengi wa vijana! wa sasa; watu tegemezi, wasio na uti wa mgongo!
Sioni vijana waliojisimamia tukapata uhuru. Sioni vijana aggressive.


Nimeshaandika hapa kuna kijana mmoja tu mwenye maono na mbunifu katika serikali hii. Hata uwaziri mkuu apewe wakati tunangojea kumkabidhi nchi.
Sijamsikia kwenye uchafu wowote, lakini madelu mara wakamatwe na wake za watu wa kampeni, mara uchawi kha.

HUSSEIN MOHAMED BASHE! Apewe uwazir mkuu haraka sana
 
Haya ndio madhara ya kuwachekea wapuuzi
 
Inasikitisha sana
 
Kipindi cha JPM miradi kibao ilisonga mbele bila Tozo...
Mi nawakumbusha tuu kuwa mwezi huu walisema Treni ya Umeme inaanza kazi.

Na hata Juzi Tarura walisaini mikataba ya barabara za vijijini cha kushangaza bara bara yetu ya Ubena to Nger haija guswa na wala hawana mpango hadi hivi sasaaa
 
Nchi haiwezi kujengwa kwa tozo. Nchi inajengwa kwa kodi inayotokana na uzalishaji, jinsi uzalishaji unavyoongezeka ndiyo na kodi inaongezeka. Tozo kwa wananchi maskini kwenye shughuli ambazo siyo za uzalishaji ni kuendeleza umaskini. Unamtumia mtu kijijiji shilingi elfu tano eti anakatwa tozo kujenga nchi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…