Prince Dube ajiondoa katika mitandao ya kijamii

Prince Dube ajiondoa katika mitandao ya kijamii

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
2,060
Reaction score
5,648
Siku moja baada ya kuibeba Yanga SC kwa bao la dakika za majeruhi dhidi ya TP Mazembe, mshambuliaji Prince Dube amejiondoa katika mitandao ya kijamii.
IMG_1634.jpeg

Hatua hiyo imewashangaza mashabiki na kuibua maswali mengi, hasa ikizingatiwa mchango wake katika kuokoa matumaini ya Yanga kwenye michuano ya CAF.

Dube, ambaye alikuwa hajafunga katika mechi 13 mfululizo, alifufua matumaini ya Yanga katika dakika za mwisho kwa goli lake la kusawazisha, lakini siku moja baadaye, akaunti zake za mitandao ya kijamii hazikupatikana tena.
photo-output.png

Hakukuwa na tamko rasmi kutoka kwa Dube kuhusu sababu za uamuzi huo, hali ambayo imeacha mashabiki wakitafakari.
 
Wamtukanee wee halafu kafunga ndo wamuone mzuri...hataki unafiko
 
Back
Top Bottom