Prince Dube: Shujaa asiyeimbwa

Prince Dube: Shujaa asiyeimbwa

MAKULUGA

JF-Expert Member
Joined
Jan 21, 2011
Posts
7,828
Reaction score
10,527
Kuna kitu kimoja kwenye soka la Tanzania! Soka ni Simba na Yanga!

Maamuzi, uendeshaji, uratibu, mipango nk yote inategemea /inahusu siasa za Simba na Yanga. Hii ni hatari kwa mustakabali wa Soka letu!

Chukulia mfano mdogo wa nyota wa Azam hivi sasa, Dube.

Huyu ni Striker hatari, lakini hajulikani. Tangu ligi ianze anafunga kila mechi so chochote mbele ya akina Mutombo, Mugalu, Bwalya au Morrison.

Tatizo so lingine bali ni Timu anayochezea!

Angekuwa yupo Simba au Yanga sasa hivi tungekuwa na watoto kadhaa wanaoitwa Prince Dube.

Sijui tatizo letu ni nini!
 
Vibe ya Simba na Utopolo haiepukiki kwa hapa bongo,ukute prince Dube yupo Azam lakini ukimuuliza kwa bongo anapenda timu gani atakwambia Simba Sports Club au Manyani/Hawajielewi fc.
 
Na usiku huu katupia Mawili. Azam Mwaka huu ni Moto wa Gesi
 
Yaani eti yule Calino ni maarufu kufika Dube

"Kama humpendi Carinhos (Lowassa), kale malimao" in Gwajima's voice!! Dah long time kitambo in 2015! Enzi hizo Gwajima yuko Chadema.
 
Kuna kitu kimoja kwenye soka la Tanzania! Soka ni Simba na Yanga!

Maamuzi, uendeshaji, uratibu, mipango nk yote inategemea /inahusu siasa za Simba na Yanga. Hii ni hatari kwa mustakabali wa Soka letu!

Chukulia mfano mdogo wa nyota wa Azam hivi sasa, Dube.

Huyu ni Striker hatari, lakini hajulikani. Tangu ligi ianze anafunga kila mechi so chochote mbele ya akina Mutombo, Mugalu, Bwalya au Morrison.

Tatizo so lingine bali ni Timu anayochezea!

Angekuwa yupo Simba au Yanga sasa hivi tungekuwa na watoto kadhaa wanaoitwa Prince Dube.

Sijui tatizo letu ni nini!
Mkuu kwani kasajiliwa lini kaonyesha uwezo lini ulitaka aanze kuimbwa lini??Msemo wa Shujaa asiyeimbwa ni MTU anayefanya vizuri kwa muda mrefu tu lakini wanasifiwa wengine.Dube wa Juzi tu hajafika hata Mechi 10.Ataimbwa tu .....by the way tumeshaanza kumuimba
 
Back
Top Bottom