Priscilla Kashakuwa Mswahili Wabongo Mtakoma; Aweka Historia Usiku wa Hina wa Zuchu, Akicheza Kibao Kata

Jannatul Firdaus

JF-Expert Member
Joined
Aug 4, 2026
Posts
446
Reaction score
1,113
Mrembo Priscilla, ambaye pia ni mke wa mwanamuziki maarufu nchini Juma Jux, ameonekana akicheza Kibao Kata. Tukio hilo lilijiri kwenye sherehe ya Usiku wa Hina iliyoandaliwa na msanii Zuchu, sherehe iliyokusanya safu ndefu ya wasanii, staa na watu maarufu wa tasnia ya burudani nchini Tanzania.

Tofauti na matarajio ya wengi waliomchukulia kama mgeni wa tamaduni hizo, Priscilla alijumuika na watu wengine kucheza kibao kata.

Mashabiki na wadau wa burudani kwenye mitandao ya kijamii kama Instagram na TikTok hawakubaki nyuma; video za mrembo huyo zimesambaa kwa kasi kubwa huku maelfu ya watumiaji wa mitandao wakikiri kuwa Priscilla ameshakuwa "Mbongo kamili" na kwamba hakuna tena cha kumfundisha kuhusu utamaduni wa Swahili.
Your browser is not able to display this video.
 
wa igbo na kukata kiuno ni utamaduni wao
 
Hili jukwaaa lina wenyewe, nimepita tu mara moja moja
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…