Prison Break vs Breaking Bad

Prison Break ni Series bora ya muda wote
 
Mkuu, embu nipe intro kidogo ya hiyo Breaking Bad.
 
Kesho nainza season 2 ya Breaking Bad,Prison Break season 2 nishaiangalia,hivyo nitarudi pia kutoa mrejesho.
2014 niliangalia S01E01 ya The Breaking Bad nikaona naangalia series ya kiboya nikaachana nayo, 2018 nikaamua kuangalia tena kwa kuwa sikuwa na series ya kuangalia, Aisee nilijilaumu sana na kujiona mjinga kukaa na mzigo mkali muda wote bila kuangalia badala yake nikawa naangalia mizigo mibovu kama MONEY HEIST. Endelea kuangalia Breaking Bad utakuja kuipa ratings kama ulizoziona mtandaoni.
 
Nipe intro kidogo kaka ya hiyo Series
 
Nipe intro kidogo kaka ya hiyo Series
Mwalimu wa Sekondari wa somo la Kemia mwenye mtoto wa kiuke mlemavu wa miguu na mke mwenye ujauzito wa bahati mbaya (unwanted pregnancy) anagundulika kuwa ana Kansa ya Mapafu na ipo steji ya juu kiasi kwamba haiwezi kutibika, amebakiza miezi 6 tu ya kuishi. Akijicheki ni kuwa hana chochote cha kuiachia familia yake pindi atakapokufa, anawaza kupambana walau apate ada ya wanawe iwasaidie kufika chuo kikuu, sasa kwa muda wa miezi 6 kupata pesa hiyo anaona hakuna njia ya mkato zaidi ya kuuza unga (madawa ya kulevya).

Anakutana na mwanafunzi wake wa zamani ambaye sasa ni muuza madawa na wanakuwa partners, mwalimu akitumia utaalamu wake wa kemia kutengeneza madawa na kijana mwanafunzi akitumia uzoefu wa mtaa kuyauza, na wakati huohuo mwalimu anapambana kujiuguza kansa kwa fedha ya madawa. Mwalimu anakuja kuwa mtengenezaji namba 1 wa madawa gredi kali na anapata hela za kufa mtu, ila sasa biashara inambadilisha tabia anakuwa mkatili na muuaji wa ajabu kabisa kwa ajili ya kulinda biashara na kumlinda partner wake. Angalia uone jinsi maisha yanavyoweza kubadilika, mwalimu muoga wa kemia kuja kuwa Drug Lord anayeogopwa na wauza madawa ya kulevya.
 
Alafu mtu sijui anatokea wapi huko anakuja kuanzisha Uzi kuwa prison Break ni series bora kuliko Breaking bad...! Aisee kweli maajabu hayakuja kuisha katika dunia hii
 
Alafu mtu sijui anatokea wapi huko anakuja kuanzisha Uzi kuwa prison Break ni series bora kuliko Breaking bad...! Aisee kweli maajabu hayakuja kuisha katika dunia hii
Oya prison break ni kali ila sio masterpiece kwa kiwango cha kuzipiga gap show kali ni vile tu ilipewa airtime yakutosha waliipromote sana kipindi kile inatoka kwaiyo tulikua tunaona hakuna mzigo mkali kuliko prison break ila sio kweli
 
Swala la series bora ni subjective, binafsi sikuipenda breaking bad, na niliishindwa GOT
Naelewa mkuu na wala sio series tu bali vitu vingine pia, ata uzuri wa mwanamke pia upo subjective ila haiwezi kuondoa ukweli kwamba msichana Fulani ni mzuri ata kama we kwako unaona ni hafai

Sasa ukiacha na Mambo ya subjective na kuongelea uhalisia haiko hivo, ukiskia watu wanasema kuwa, Watanzania wenye Asili ya mkoa wa Kigoma ni wafupi sio kwamba na warefu waga hawapo, warefu wapo ila ni wachache na wafupi ndio wengi

Kwahiyo ukiona Katika watu 100, 95 Kati ya hao wanasema kitu Fulani ni kizuri na hao wa5 wanasema kibaya basi shida haipo kwa wale 95 bali kwa hao 5

Kwahiyo haiwezekani waangalia movie wengi waliopo Duniani waseme movie Bora ya mwaka 2022 labda ni NOBODY alafu wachache wakatae basi nasie tuungane nao, haiwezekani kubadiri mawazo ya wengi japokuwa tutaheshimu pia mawazo ya wachache
 
Uko sahihi
 
Swala la series bora ni subjective, binafsi sikuipenda breaking bad, na niliishindwa GOT
Ni kweli kabisa. Vipi kuna uwezekano kuwa hukuziangalia mpaka mwisho hizo series? Yaani BB na GOT
 
Walter alikuwa ana akili za kiwango cha juu sana, ingawa waliomzunguka (ikiwa ni pamoja na mke wake SKYLER) walikuwa wanamwona mtu wa kawaida mno. Lilikuwa ni somo pia kuwa mtu anaweza kuishi chini ya uwezo wa akili yake na akawa maskini kabisa ilhali alikuwa na uwezo wa kuwa bilionea. Imagine Walter angeamua kuwa mtengeneza madawa akiwa na miaka 35 hivi, angekuwa level za kina Don Eladio na Gus Fring kwa utajiri
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…