Mwalimu wa Sekondari wa somo la Kemia mwenye mtoto wa kiuke mlemavu wa miguu na mke mwenye ujauzito wa bahati mbaya (unwanted pregnancy) anagundulika kuwa ana Kansa ya Mapafu na ipo steji ya juu kiasi kwamba haiwezi kutibika, amebakiza miezi 6 tu ya kuishi. Akijicheki ni kuwa hana chochote cha kuiachia familia yake pindi atakapokufa, anawaza kupambana walau apate ada ya wanawe iwasaidie kufika chuo kikuu, sasa kwa muda wa miezi 6 kupata pesa hiyo anaona hakuna njia ya mkato zaidi ya kuuza unga (madawa ya kulevya).
Anakutana na mwanafunzi wake wa zamani ambaye sasa ni muuza madawa na wanakuwa partners, mwalimu akitumia utaalamu wake wa kemia kutengeneza madawa na kijana mwanafunzi akitumia uzoefu wa mtaa kuyauza, na papo hapo mwalimu anapambana kujiuguza kansa kwa fedha ya madawa. Mwalimu anakuja kuwa mtengenezaji namba 1 wa madawa gredi kali na anapata hela za kufa mtu, ila sasa biashara inambadilisha tabia anakuwa mkatili na muuaji wa ajabu kabisa kwa ajili ya kulinda biashara na kumlinda partner wake. Angalia uone jinsi masiha yanavyoweza kubadilika, mwalimu muoga wa kemia kuja kuwa Drug Lord anayeogopwa na wauza madawa ya kulevya.