Prison Break vs Breaking Bad

Prison Break vs Breaking Bad

Mwalimu wa Sekondari wa somo la Kemia mwenye mtoto wa kiuke mlemavu wa miguu na mke mwenye ujauzito wa bahati mbaya (unwanted pregnancy) anagundulika kuwa ana Kansa ya Mapafu na ipo steji ya juu kiasi kwamba haiwezi kutibika, amebakiza miezi 6 tu ya kuishi. Akijicheki ni kuwa hana chochote cha kuiachia familia yake pindi atakapokufa, anawaza kupambana walau apate ada ya wanawe iwasaidie kufika chuo kikuu, sasa kwa muda wa miezi 6 kupata pesa hiyo anaona hakuna njia ya mkato zaidi ya kuuza unga (madawa ya kulevya).

Anakutana na mwanafunzi wake wa zamani ambaye sasa ni muuza madawa na wanakuwa partners, mwalimu akitumia utaalamu wake wa kemia kutengeneza madawa na kijana mwanafunzi akitumia uzoefu wa mtaa kuyauza, na wakati huohuo mwalimu anapambana kujiuguza kansa kwa fedha ya madawa. Mwalimu anakuja kuwa mtengenezaji namba 1 wa madawa gredi kali na anapata hela za kufa mtu, ila sasa biashara inambadilisha tabia anakuwa mkatili na muuaji wa ajabu kabisa kwa ajili ya kulinda biashara na kumlinda partner wake. Angalia uone jinsi maisha yanavyoweza kubadilika, mwalimu muoga wa kemia kuja kuwa Drug Lord anayeogopwa na wauza madawa ya kulevya.
umeielezea vizur
tangu nilipoona hii kitu seriees zingine naona wanapotez muda tu
 
OZ kali sana, The Wire niliishia Season 2 ngoja nianze upya niiangali mpaka mwisho..dogo Marlow aliwahangaisha wakongwe hawakuamini.. The Sopranoz ndio naangalia sasa hivi season 1, hii ninayo complete nimeichukua majuzi hapa...Six Feet Under ngoja niitafute..mizigo ya zamani mitamu sana
Noma sana mizigo ya kiutu uzima hiyo heavy sana
 
Angalia moja ya kituruki inaitwa "Eskiya Dunyaya Hukumdar Olmaz(EDHO)" yaani "Bandits will never rule the World", utakuja kunishukuru...
Hiyo ndo criminal series kali kwangu kuliko hizo zako amini.
Pia utaongezea na "Sons of Anarchy"
uzi unahusu breaking bad na prison break sasa utaletea mambo mengine hapa
 
Series za HBO ya mwanzo mwanzo huwezi fananisha na hizi za siku hizi.. my first tv show to fall in love with was prison break but nikaja kugundua kuna vitu vikali sana hata kabla ya prison break na baada pia...

Cheki the wire... sopranos.. OZ.. six feet under
Oz iko poa sana....inaonyesha uhalisia wa gereza kabisa
 
Prison break ya kitoto sana. Kama tu ilivyo Lost. Huwezi fananisha na Breaking Bad. Braking bad ni level za The Sopranos.
 
Mkuu The Knowledge Seeker nimeamua kupoteza muda kuitazama ili nijiridhishe maana nimekuwa nikisema Hakuna Series kali kama Prison Break ila naishia kutukanwa kwamba sizijui series kali na wanasema bila kupepesa Macho ya kwamba Breaking Bad ni bonge moja la series,ndiyo maana nataka ninihakikishie halafu nitakuja na conclusion,Mpaka sasa kwa hizi season 1 kila upande,kwakweli PRISON BREAK naipa 10/10 na hiyo BREAKING BAD naipa 2.9/10.
Jamani PB ni nzuri mnoo...aisee wale watu mpk nikawa nawaota...yani wote ni wakali kwenye kila scene zao wamezitendea haki...unaweza irudia na usichoke kama movie ya Sarafina
Ngoja na mm niitafute hyo BB...
 
Prison break ya kitoto sana. Kama tu ilivyo Lost. Huwezi fananisha na Breaking Bad. Braking bad ni level za The Sopranos.
Umenikumbusha na hii kitu LoST duuh nilikua naunguza msosi..I was addicted
 
Nisikuchoshe na usinichoshe,tusichoshane!.

Mimi ni mdau wa series hasa za crime & drama, sasa baada ya kuitazama series ya Prison Break kwa kuirudia mara kadhaa na kujiridhisha kwa mambo kadhaa, kiukweli nimekuwa nikipata tabu sana kuangalia series nyingine kali kushinda Prison Break, sasa kila mtu(wataalamu wa series na wasio wataalamu)ninapomuuliza series gani kali kushinda Prison Break wamekuwa waki -recomend niangalie series ya Breaking Bad kwani ni bonge moja la series Kushinda Prison Break na kwenye viwango ina ratings kubwa kushinda Prison Break.

Leo nimeianza rasmi Breaking Bad na nitakuwa naleta mrejesho ili nione mimi mwenyewe ipi ni series bora na kali.

Kwa sasa nimeangalia Breaking Bad season 1 na nilishaangalia Prison Break season zote,sasa leo nitafanya comparison kwa season 1 kila upande.

Nitagawa ratings kwa hizi season 1 za hizi series zote mbili.(Ratings itakuwa kuanzia 1 - 10)

1.PRISON BREAK SEASON 1 NAIPA 10/10

2.BREAKING BAD SEASON 1 NAIPA 2.9/10.

Kesho nainza season 2 ya Breaking Bad,Prison Break season 2 nishaiangalia,hivyo nitarudi pia kutoa mrejesho.

Kazi imeanza
usijichoshe ngoja nikupe summary apa
Prison break season 1 ndo season kali storyline waliua sana ila kuanzia seadon 2 na kuendelea walizngua
Breaking Bad kuanzia season 1 mpaka season 3 ni mbaya storyline ni ya kawaida ya kitoto sana,kidogo wakaja kujitahidi kwene season 4 na 5 ndo wamejitahidi kidogo,ila yote kwa yote sio nzuri.
NB; Ukitaka series yenye storyline kali icheki power mzigo kuanzia season mpaka mwisho season 5 nahisi ni moto tu
 
Power Yenye Ngono Tu?
 
Ni bora umesema, UNAHISI.
 
Back
Top Bottom