Privacy Law: Mwanaasha J. Kikwete kuwashitaki NECTA?


Umemjibu vyema hata kama sio mwanasheria kwa taaluma
Ila mto amada afikirie maana alichokiweka hapo ni poor interpretation of the law and wrong definition ya privacy

Kuna sehem nyingine huwa haiaply na inapobidi hata kama ni suimu yako ya mkononi uhuru huo unaingiliwa na kuvunjwa
So katika mazingira haya NECTA haijaingilia uhuru wa mhusika wala kuvunja sheria inayohusiana na privacy
 
napita hapa_maake panahitaji uelewa wa sheria ili kuchangia....ntarudi kama msomaji tu.
 
Mbona watahiniwa wote majina yao na matokeao yao vimewekwa wazi? whats wrong na huyu mtoto?.......ingawa klam mzazi sijapenda barrage of criticism aliyoipata hapa JF...

ndio gharama ya kuwa "public figure" siye kapuku nani anatujua hata ukiweka majina yetu na division x zetu!
 
Wrong definition of Law!

One of the key subject functions of the NECTA is to disclose the names and results of students!

Haven't you found in this thread, a place to squeeeze your religious segregation mr MS?
duhu..............
 
Eti ehhh! Ingekuwa Ugonjwa labda lakini majibu ya mtihani!
Hivi hawa first families si wanatakiwa kuwa role models? Kama anafeli na huku tunawalisha na kuwalaza bure, wanapata priviledges kibao, mama ni mwalimu by profession - something must be very wrong with this family!
 
Kupata alama za chini hakumaanishi hana akili wala hakumaanishi hajiwezi kimasomo.

Ni mambo mengi mno yanayoweza kupelekea mtu kupata alama za chini katika mtihani.

Kuna watu wana vifesti klasi vyao vya UDSM na hata kifutio hawajawahi kuvumbua! So go figure.
 
kwa hilo wote waliofeli wangeishtaki NECTA kitambo sana..
 
Ha ha ha ha ha ha! Usishangae akawa beneficiary No. 1 wa HESLB wakati mtoto wa mkulima aliyesomea chini ya mawe na kadivisheni II kake akaambiwa ha-qualify kwa loan! Hii nchi bana!
 
unasoma au umesoma law wapi? degree?masters?phd?
 
Kwa nini usimshauri abadilishe jina? Labda itasaidia kumwongezea akili
 
Ukiwa kenge hata tafakuri inakaa mkiani
 

Inaonekana waliokujibu hawakukujibu kwa kutumia sheria. Kwa hiyo mimi nitakujibu kwa kutumia sheria. Kabla ya kukujibu inabidi ujue kwamba, any article in the Constitution should not be read in isolation of the others. Pia inabidi ujue kwamba, Ibara nyingi za Katiba ya sasa zinaanza na "Bila kuathiri sheria nyingine za nchi........" Katiba inakupa haki kwa mkono wa kulia, then inaichukua haki hiyo hiyo kupitia mkono wa kushoto.

Now kukujibu hoja yako. Ni kweli Katiba inatoa haki ya privacy. Hata hivyo, ibara ya 30(2) ya Katiba hiyo hiyo inasema "Ifahamike kwamba masharti yaliyomo katika Sehemu hii (sehemu ya tatu ya haki za binadamu) ya Katiba hii, yanayofafanua misingi ya haki, uhuru na wajibu wa binadamu, hayaharamishi sheria yoyote iliyotungwa wala kuzuia sheria yoyote kutungwa au jambo lolote halali kufanywa kwa mujibu wa sheria hiyo..." I am sure NECTA watakuwa wana-publish majina ya wanafunzi waliofaulu na kufeli kwa mujibu wa sheria iliyotungwa na bunge.

Kwa kifupi vyombo vya dola viliyo chini ya serilkali inayoongozwa na baba yake vimekuwa vikitumia sana hiki kifungu kukandamiza haki za binadamu. Unaenda mahakamani una-cite haki yako ya kibinadamu jamaa wana-cite Ibara ya 30(2) na kesi unashindwa. Kwa hiyo, mtoto wa kikwete ni victim wa katiba mbovu kama wananchi wengine. She is not an exception. Anachotakiwa kufanya sasa ni kumshauri baba yake ili Ibara ya 30(2) indolewe kabisa kwenye Katiba mpya ili yasije yakampata tena.

Kwa hiyo, hii ni changamoto kubwa sana kwake kuona jinsi Katiba ilivyo mbovu. Inambidi sasa nae kuwa mstari wa mblele kabisa kupigania Katiba mpya inayolinda sio tuu privacy yake bali pia privacy za Watanzania wote. Thus, wa kumlaumu sio NECTA bali ni baba yake aliyekubali kuongoza hii nchi kwa katiba ambayo haijali haki za binadamu including hata haki za watoto wake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…