Inaonekana waliokujibu hawakukujibu kwa kutumia sheria. Kwa hiyo mimi nitakujibu kwa kutumia sheria. Kabla ya kukujibu inabidi ujue kwamba, any article in the Constitution should not be read in isolation of the others. Pia inabidi ujue kwamba, Ibara nyingi za Katiba ya sasa zinaanza na "Bila kuathiri sheria nyingine za nchi........" Katiba inakupa haki kwa mkono wa kulia, then inaichukua haki hiyo hiyo kupitia mkono wa kushoto.
Now kukujibu hoja yako. Ni kweli Katiba inatoa haki ya privacy. Hata hivyo, ibara ya 30(2) ya Katiba hiyo hiyo inasema "Ifahamike kwamba masharti yaliyomo katika Sehemu hii (sehemu ya tatu ya haki za binadamu) ya Katiba hii, yanayofafanua misingi ya haki, uhuru na wajibu wa binadamu, hayaharamishi sheria yoyote iliyotungwa wala kuzuia sheria yoyote kutungwa au jambo lolote halali kufanywa kwa mujibu wa sheria hiyo..." I am sure NECTA watakuwa wana-publish majina ya wanafunzi waliofaulu na kufeli kwa mujibu wa sheria iliyotungwa na bunge.
Kwa kifupi vyombo vya dola viliyo chini ya serilkali inayoongozwa na baba yake vimekuwa vikitumia sana hiki kifungu kukandamiza haki za binadamu. Unaenda mahakamani una-cite haki yako ya kibinadamu jamaa wana-cite Ibara ya 30(2) na kesi unashindwa. Kwa hiyo, mtoto wa kikwete ni victim wa katiba mbovu kama wananchi wengine. She is not an exception. Anachotakiwa kufanya sasa ni kumshauri baba yake ili Ibara ya 30(2) indolewe kabisa kwenye Katiba mpya ili yasije yakampata tena.
Kwa hiyo, hii ni changamoto kubwa sana kwake kuona jinsi Katiba ilivyo mbovu. Inambidi sasa nae kuwa mstari wa mblele kabisa kupigania Katiba mpya inayolinda sio tuu privacy yake bali pia privacy za Watanzania wote. Thus, wa kumlaumu sio NECTA bali ni baba yake aliyekubali kuongoza hii nchi kwa katiba ambayo haijali haki za binadamu including hata haki za watoto wake.