Privacy my foot! Wanafunzi wangapi majina yao yameanikwa ije kuwa huyu mbumbumbu?!!
Hapa ulichofanya, huja address issue ya privacy. Umei dismiss. Umeihalalisha kwa sababu privacy imevunjwa kwa wote.
Hujasema kwamba lack of privacy ni nzuri au mbaya.
Ni kama vile mtu mmoja akilalamika kwamba mtoto wake kauawa katika genocide ya Rwanda halafu wewe ukaja kusema "genocide my foot, wangapi wameuawa uje kusema wewe tu"
Two wrongs don't make a right. Kitu kibaya ni kibaya tu, kikifanyika kwa mtu mmoja au wengi. Tatizo ni kile kitu nilichokisema mwanzo, wabongo wengi tunaogelea katika maji ya kukosa privacy. Hewa tunayoivuta imechafuliwa na kukosa privacy na wala hatujui hili.
Bongo si ajabu mtu kukosa concept ya personal space na kukuongelesha all up in your face!! Hatuna sense of privacy.
Wewe mtu anakaa chumba kimoja na baba na mama yake pamoja na wadogo zake watatu, chumba kimepigwa pazia upande wa pili wanalala baba na mama. Huyu by default ukimwambia kwamba matokeo ya mtihani yanatakiwa kuwa private hawezi kukuelewa.
Kwa sababu nyumbani hata baba anapomjua mama hakuna privacy. Maybe this is an extreme example, lakini ukweli ni kwamba wengi tunaishi / tumeishi katika small variations za hilo. Kwa hiyo ndiyo maana ni rahisi kusema "privacy my foot". Si utamaduni wetu!
Mtu anaoga choo cha passport size ukipita nje unamuona, leo unataka kumwambia matokeo ya mtihani yanatakiwa kuwa private atakuelewa vipi?
Ndiyo predicament yetu wabongo hii. Naona watu wanaongelea sana sheria, ni vizuri. Lakini sheria bila utamaduni tutabaki na sheria kwenye vitabu.
Kinachotakiwa hapa ni kuimarisha uchumi na kubadili utamaduni.