Privaldinho amjibu Oruma

Frank Wanjiru

JF-Expert Member
Joined
Apr 12, 2012
Posts
22,719
Reaction score
40,739
Ndugu yangu Oruma unaijua Mamelodi ya miaka 7,?? Ndio Mamelodi iliyobeba ubingwa? Pengine hujawaelewa mashabiki wa Mamelodi. Nafikiri Mashabiki wa Mamelodi wameona namna mradi wa Eng @caamil_88 unavyoshamiri.

Salaam Bw Oruma

Wanaposema wanaiona Yanga kama Mamelodi ya miaka 7 iliyopita wanaiona Yanga SC hatari bora na yenye malengo makubwa miaka 7 iliyopita. Sidhani kama wanaikebehi na kuikejeli kama baadhi ya wachambuzi na waandishi wanavyofanya. Wanaheshimu mradi wetu.

Tunajua Mamelodi wana dhamira gani. Tunajua wapi wamekwama katika kipindi cha miaka 7. Ukiitazama Mamelodi ukiachana msimu uliopita imekwama robo fainali miaka minne mfululizo.

2021/22 walitolewa na Petro Luanda
2020/21 walitolewa na Al Ahly
2019/20 walitolewa na Al Ahly

Katika kipindi cha miaka 7, Mamelodi haijawahi kuingia fainali ya ligi ya Mabingwa isipokuwa kutinga hatua ya nusu fainali mara mbili. Maana yake nini? Wana mission ambayo haijakamilika.

Unafikiri Rhulan hataki kuvaa viatu vya Pitso? Tunajua ndio dhamira yake, lakini je Gamondi anataka kutembea peku ? Nae ana viatu vyake anataka kuvivaa.

Tulishatoa ujumbe wetu Shirikisho kwa akina Mazembe na wengineo, huku kwa mabingwa nako tuna salam zetu. Hatujaja kushiriki kwa kutazama historia za watu. Nasi tumekuja kuandika historia yetu.

Kwa bahati mbaya sana Yanga ipo Tanzania sehemu ambayo watanzania wenyewe hatupendi kuona project zetu zikikua.

Mijadala iliyopo kwenye media ni za kutishana na kuishusha Yanga pasi na kuuheshimu mpira wa miguu.

Tumesahau msimu wa kwanza Teungeth kwenye ligi ya mabingwa waliiondoa Raja Casablanca, ?? Tumesahau juzi tu Wydad ameshindwa kufuzu mbele ya kundi la vibonde kwake ukilinganisha mafanikio yake?

Tumesahau leo hii Berkane na Raja hawapo mashindano ya kimataifa?. Msimu uliopita Berkane hakutinga hatua yoyote ya makundi baada ya kuondolewa na Monastir ambayo katika historia ya soka lao ilishiriki kwa mara ya kwanza CAF mwaka 2019?

Sayansi ya soka haingopi wala haitishwi na siasa za mpira kama kuna mradi makini na wenye malengo. Tunaiheshimu Mamelodi na tunajua ni mchezo mgumu sana lakini tunaheshimu zaidi mradi wetu

Salaam Oruma.

 
Wanaposema wanaiona Yanga kama Mamelodi ya miaka 7 iliyopita wanaiona Yanga SC hatari bora na yenye malengo makubwa miaka 7 iliyopita. Sidhani kama wanaikebehi na kuikejeli kama baadhi ya wachambuzi na waandishi wanavyofanya. Wanaheshimu mradi wetu.
Kwa hiyo hapo ni suala la kupishana tafsiri tu kati ya Oruma na Privadinho kuhusu matamshi ya mashabiki wa Mamelodi, lakini aliyetoa kauli wanabaki kuwa ni mashabiki wa Mamelodi
 
Mtatokea wapi na kwa figisu gani?

Mkisema mcheze saa 9 alasiri muwakomeshe kwa jua kali mtagundua hiyo mbinu haiwezi kufanya kazi.

Hususani pale unapokumbuka Al Ahly alipochezea goli 5-0 ilikuwa ni mechi iliyochezwa muda huo huo saa 9.

Mnapata wazo labda muwekeze focus kwa Sangoma, mechi muimalizie huko.

Mnagundua kazi ya Sangoma wa Yanga ni kuwafanya wapinzani wawe wanaona giza.

Wakati mnafurahia hilo na kuona mwanga wa matumaini ghafla mnasikia meseji ya muamala, Sangoma karudisha hela.

Wakati mnashangaa kwanini Sangoma arudishe hela, mnastukia meseji ya Sangoma WhatsApp.

Kufungua meseji mnakutana na hii clip.
Your browser is not able to display this video.
 
Oruma yupi huyo? Wilson Oruma, please,! Toka lini mashabiki wakacheza mechi? Huwezi kuona kocha au mchezaji professional anadharau timu pinzani. Bongo peke yake ndiyo kuna huu upuuzi. Oruma ni mchambuzi? Hakuna wachambuzi hapa ni mashabiki uchwara tu.
Nilishamwona Oruma toka enzi zile nafikiri ilikuwa Channel ten ya sasa. A total joke.
Ndiyo maana huwa sipendi kuangalia mechi kwenye local channels because I love the beautiful game.
A a
 
Cc tunajua kutunza risiti tu muda ni mwalim mzuri
 
Mara ya mwisho Mamelody sundown kuchukua kombe la Africa ilikua mwaka elfu mbili na kumi na sita(2016).Miaka saba nyuma sasa mashabiki kama wanaifananisha Yanga na Mamelody sundown ya miaka saba iliyopita basi wanaitamka Yanga tishio na yenye kujua mpira kama ilivyokua Mamelody sundown ya 2016 iliyotwaa ubingwa wa Cafcl league.
 
Kama mnajua Mamelodi alitolewa mara kadhaa robo fainali, pamoja na kiwango alichokuwa nacho, kwanini mnaikebehi Simba kutolewa robo fainali mara kadhaa Sasa?
Simba lazima ikebehiwe ndio soccer letu yani unataka tuipongeze Simba!?tafadhari kunywa juice ya moto Simba robo ndio kombe lao kwa Caf
2006 Mamelody alichukua kombe
 
Muda si mrefu utameza haya matapishi yako ya vingwendu kama ulivyomeza kwa Belouzdad
 
Simba lazima ikebehiwe ndio soccer letu yani unataka tuipongeze Simba!?tafadhari kunywa juice ya moto Simba robo ndio kombe lao kwa Caf
2006 Mamelody alichukua kombe
Kwa hiyo unaungana na Oruma kusema kwamba Mamelodi ni timu hatari sana, na unapingana na Privadinho anayesema hivyo ni vitisho tu?
 
Yeye mwenyew hajaheshimu mpira kusema wydad ameshindwa kufuzu kwenye kundi la vibonde ety berkane hayupo kwenye mashindano ya kimataifa duuuuuhhh
 
Yanga haijawahi kutegemea Jua ili kuwafunga wapinzani hata game ya Belouizdad ambao ndio waarabu wanaogopa Jua tuliwachezesha usiku ili tukiwapige wasiwe na visingio vya jua au joto....

Kuhusu ushirikina kila mtu anajua timu inayoroga mchana kweupe ni Kolo wizards maana mlichoma madawa yenu Kule south Hadi mkapigwa faini....

Yanga ni soka Safi ndo linatubeba... Ningekuaona mjanja kama ungesema mapema Mamelodi sundown n Bora au yupo unga
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…