Frank Wanjiru
JF-Expert Member
- Apr 12, 2012
- 22,719
- 40,739
Ndugu yangu Oruma unaijua Mamelodi ya miaka 7,?? Ndio Mamelodi iliyobeba ubingwa? Pengine hujawaelewa mashabiki wa Mamelodi. Nafikiri Mashabiki wa Mamelodi wameona namna mradi wa Eng @caamil_88 unavyoshamiri.
Salaam Bw Oruma
Wanaposema wanaiona Yanga kama Mamelodi ya miaka 7 iliyopita wanaiona Yanga SC hatari bora na yenye malengo makubwa miaka 7 iliyopita. Sidhani kama wanaikebehi na kuikejeli kama baadhi ya wachambuzi na waandishi wanavyofanya. Wanaheshimu mradi wetu.
Tunajua Mamelodi wana dhamira gani. Tunajua wapi wamekwama katika kipindi cha miaka 7. Ukiitazama Mamelodi ukiachana msimu uliopita imekwama robo fainali miaka minne mfululizo.
2021/22 walitolewa na Petro Luanda
2020/21 walitolewa na Al Ahly
2019/20 walitolewa na Al Ahly
Katika kipindi cha miaka 7, Mamelodi haijawahi kuingia fainali ya ligi ya Mabingwa isipokuwa kutinga hatua ya nusu fainali mara mbili. Maana yake nini? Wana mission ambayo haijakamilika.
Unafikiri Rhulan hataki kuvaa viatu vya Pitso? Tunajua ndio dhamira yake, lakini je Gamondi anataka kutembea peku ? Nae ana viatu vyake anataka kuvivaa.
Tulishatoa ujumbe wetu Shirikisho kwa akina Mazembe na wengineo, huku kwa mabingwa nako tuna salam zetu. Hatujaja kushiriki kwa kutazama historia za watu. Nasi tumekuja kuandika historia yetu.
Kwa bahati mbaya sana Yanga ipo Tanzania sehemu ambayo watanzania wenyewe hatupendi kuona project zetu zikikua.
Mijadala iliyopo kwenye media ni za kutishana na kuishusha Yanga pasi na kuuheshimu mpira wa miguu.
Tumesahau msimu wa kwanza Teungeth kwenye ligi ya mabingwa waliiondoa Raja Casablanca, ?? Tumesahau juzi tu Wydad ameshindwa kufuzu mbele ya kundi la vibonde kwake ukilinganisha mafanikio yake?
Tumesahau leo hii Berkane na Raja hawapo mashindano ya kimataifa?. Msimu uliopita Berkane hakutinga hatua yoyote ya makundi baada ya kuondolewa na Monastir ambayo katika historia ya soka lao ilishiriki kwa mara ya kwanza CAF mwaka 2019?
Sayansi ya soka haingopi wala haitishwi na siasa za mpira kama kuna mradi makini na wenye malengo. Tunaiheshimu Mamelodi na tunajua ni mchezo mgumu sana lakini tunaheshimu zaidi mradi wetu
Salaam Oruma.