Probationary Employee

Probationary Employee

Joined
May 12, 2016
Posts
6
Reaction score
1
Msaada jamani wanajukwaa,

Kuna mfanyakazi wa umma kaajiriwa na barua yake ya ajira (mkataba), inasema kipindi cha majaribio ni mwaka mmoja.

Kafanya kazi mwaka 1 umeisha, mwaka wa 2,3,4 imepita mwajiri kakaa kimya hajamuongezea muda wa majaribio, hajampa barua ya kuterminate ajira, wala hajamthibitisha kazini.

Mfanya kazi huyu atakuwa na status gani kisheria? Ni haki zipi za mfanyakazi anazikosa? Madhara yake ni yapi endapo atafukuzwa kazi?

Pliz assist with statutory provisions and caselaw.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Yuko chini ya serikali za mitaa, au ni serikali kuu?
Kama ni serikali za mitaa aende kwa mkuu wake wa idara katika Halmashauri anayofanyia kazi, kupitia kwa katibu wake ataipata hiyo barua. Halmashauri zetu wanajisahau sana, hawana mpango kazi unaowakumbusha kila mfanyakazi na haki zake za msingi anazotakiwa kupewa kwa muda fulani, ni lazima uende kudai kwa nguvu


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Kama alpewa barua na mwaka ukaisha, yeye kwanza alichukua hatua gani kufuatilia barua yake ya ajira?

Aanzie hapo, akiipewa ama asipopewa ndio hoja zitaanzia hapo.

However, by mecessary implication, huyo tayari ka pass probation test na ndio maana wameendelea kuwa naye. Afuatilie barua atapewa.
 
Ukisoma Government Standing Order, ipo wazi kuwa baada ya muda wa probation kwisha, na pale ambapo mwajiriwa atamkumbusha mwajiri juu ya barua ya uthibitisho kazini; na ikiwa mwezi utapita bila ya kupewa barua ya uthibitisho, basi mtumishi huyo itachukuliwa kama amethibitishwa kazini.
 
Back
Top Bottom