Habari zenu wandugu.
Naomba kwa mwenye uelewa juu ya mikopo,maana kunasiku nimeenda NMB-Nbarali nikataka kujua utaratibu mzima wa mikopo na urejeshwaji wake kiukweli nilishangaa sana.
Pale nilipopigiwa hesabu na kuambia katika mkopo wa 10m kuna proccesing fee-kama laki mbili.Insurance fee kama 180000,ambayo mteja atakatwa katika mkopo wake.
SWALI:mteja analipa hizo fees kwa kigezo gani ikiwa bado riba atatakiwa kulipa,naomba ufafanuzi maana yule L.O alikerwa na maswali yangu kiasi cha kushindwa kunihudumia.