TANZIA Producer Geof Master aliyefanya kazi Tongwe Records afariki dunia

Kakumamoto

JF-Expert Member
Joined
May 6, 2015
Posts
1,237
Reaction score
1,696
Habari wanaburudani, nimepokea taarifa za kusikitisha za msiba wa Producer Geof Master muda huu. Naambiwa alikua kalazwa Ocean road. Mara ya mwisho kuonana nae mitaa ya Tegeta alikuwa na uvimbe puani na alikuwa kwenye harakati za kufanyiwa upasuaji.

Naambiwa leo asubuhi amefariki. Mama yake anaishi Tegeta, naamini msiba wake pia utakuwa Tegeta. Kwa mlio mjini na mkaweza kufika msibani, tunaomba muendelee kutupa taarifa zaidi. Pumzika Pema Peponi Geof Master aka Manuva.


=======

Geof Master alisimamia wimbo maarufu wa 'Zimbabwe' wa Roma Mkatoliki pia alishirikishwa kwenye wimbo wa 'Ivan' na Roma Mkatoliki.

Geof Master ameacha watoto saba kutoka kwa mama wanne.
 
Ocean Road Hospital maana yake Cancer imemuondoa.
 
R.I.P niliwah record ngoma kwake mwamba mtu poa sana, nilikuwa na k200 lakini mwamba akanitolea kitu bila malipo na ilisumbua sana ile ngoma East Africa dah pumzika salama nitaku wish sana
 
R.I.P master
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…