TANZIA Producer Geof Master aliyefanya kazi Tongwe Records afariki dunia

Geof master salute
RIP
Ndio aliyeproduce wimbo wa Zimbabwe? Sidhani
Wengi huchanganya Kati ya beat composer na anayefanya mixing. Kuna muda anayefanya mixing ndio anaonekana kapiga beat hasa pale anapokua na jina kubwa kuliko anayepiga beat
 
Roma alivyoripoti huu msiba kule Twitter aliuweka huo wimbo kwenye caption.
 
Sijaona, mm sio follower wake wala sio shabiki yake. nimeweka neno sidhani hapo kwa maana sina uhakika, sorry amesema geof master ndio ameproduce wimbo wa zimbabwe?
 
Ndio. Na hata huo wimbo ukianza anamtaja mwanzoni kabisa.
 
Screenshot_20240130-115716.jpg

TANZIA.

Pichani ni Producer wa Muziki Tanzaniq, alipozaliwa Wazazi wake walimwita Geofrey Batista Msumule, baadye alipoanza kazi za Muziki alijiita Geof Master, na pale studio ya Tongwe Rec ambapo ndo alikua akifanya kazi zake walikua wakimuita Manuva, wakimaanisha mtu mwenye Maujanja flani anapokua nyuma ya Computer akitengeneza Beats tofauti, mimi binafsi nilimuita Kingaru.

Geof Master alikua ni Rafiki, Msanii mwenzangu, mdogo wangu wa Mtaani pia.

Wapo Ma Producer wwngi ambao waliutafuta U producer kwa hari na Mali, walikua na Ndoto hizo toka zamani, wakienda Studio moja hadi nyingine, kukutana na kuwaomba Producers waliowatangalia wawafundishe Namna ya kuandaa Beats, kurecord na Muziki kwa Ujumla, kwa Geof Master hakuwahi kuwaza wala kufikiri kuwa kuna siku atakuja kuwa Producer, haikuwahi kuwa ndoto yake, ila U producer ndo ulimchagua yeye.

Miaka ya 2000 Jiji la Dar es salaam lilikua na Vijiwe vya Vijana, ambavyo viliitwa Camp, karibia kila Mtaa kulikua na Camp, vijana wenye Vipaji hasa vya Muziki ndo ilikua ni sehemu zao za kukutana, kuchangishana pesa na baadaye kwenda Studio ku record nyimbo, na siku ya Uzinduzi wa Camp zao, basi wangeimba Nyimbo zao live, ama wangealikwa kwenda kuimba kwenye Uzinduzi wa Camp nyingine, Mtaani alipotokea Geof Master napo kulikua kuna Camp mbili, moja ikiitwa Home boys Camp, hii ililua ya Kaka zake Geof, nyingine ikiitwa Marijali Camp, hii ndo ilikua Camp ya Geof, kwa sababu, marafiki wa rika lake, vijana waliosoma wote walikua kwenye hii Camp.

Geof alikua mtu wa Kanisani, akiimba Kwaya Kanisani, na akitegemewa Kupiga Kinanda Kanisani, alikua na Mwanamuziki kamiri, akipiga vyombo kadhaa vya Muziki, ila alikua Master kwenye Kupiga Kinanda, wakati Marafiki na Vijana wenzake wakiwa busy kwenye Camp yeye alikua Busy Kanisani, Marafiki na Vijana wenzake 2 wanaenda Studio moja ilokuepo Bahari beach, ikiitwa Seifii Record, wanamwambia Producer Seif kwamba walitaka aina flani ya Vinanda vipigwe kwenye Beat yao, Producer yule akawambia yeye hajui kupiga Vinanda live, ndo hapo Hao Madogo wakamkumbuka Geof Master, wakawambia Producer Seif wanaye Rafiki yao ni mpiga kinanda Kanisani, kesho yake watakuja nae ili awasaidie kuingiza hizo Vinanda.

Wale madogo wakarudi Mtaani, wakaongea na Geof Master, kesho yake safari ya Studio ikaanza, njiani Madogo wanamwimbia Geof Nyimbo yao, na kumwambia vile wanataka Kinanda kipigwe vipi, walipofika Studio, Geof kakaa kwenye Kiti cha Producer, Kinanda kipo mbele yake, akaanza Kuifanya kazi ambayo ameizoea kuifanya akiwa Kanisani, namna alivyokua anakipiga kile kinanda, yule Producer alikua akimshangaa, baada ya kumaliza kuingiza kile kinanda, na marafiki zake kuridhika, akaomba sasa aondoke kurudi Nyumbani coz muda si mrefu angetakiwa kuwepo Kwenye mazoezi ya Kwaya Kanisani.

Producer Seif anamwomba Geof wafanye kazi pamoja, Geof anamwambia lakini yeye hajui Computer, hajui kuandaa Beat, yeye anaujua tu Muziki na kupiga baadhi ya Vyombo, Seif anamwambia anamwitaji ili awe anamsaidia kuingizia Vinanda live kwenye beats za Wasanii, vingine atamfundisha, huo ukawa mwanzo wa Geof Master kuingia kwenye Ulimwengu wa kuandaa Muziki.

Moja kati ya Wasanii wakubwa ambao bila Geof ni ama angechelewa kutoka ama asingesikika ni 20%, akitoka Kimanzichana na Baiskeri mpaka Bahari ku record, ni Geof Master alikua akimtengenezea Muziki wake wakati huo hakuna mtu anayemfahamu 20%, nyimbo kama Mama Neema, Maisha ya Bongo na nyingine, zimepita kwenye mkono wa Geof Master.

Baadaye Geof Master uwezo wake ukaongezeka akaanza kwenda mikoani kufanya kazi, akianza na Mtwara, then Songea, baadaye Mbeya, na aliporudi Dar es salaam, akaanza kufanya kazi Kama Kawa Record, Studio iliyokuepo Riverside Ubungo, ambapo alifanya Nyimbo nyingi na nyingine zikawa Maarufu kama Speed 120 ya Cheed benz na Ngwair, Beef ya Ngwair n.k, baadaye Geof akaanza kufanya kazi Tongwe Records Studio iliyo chini ya J mulder. ambapo huko akafanya kazi nyingi sana, na wasanii wakubwa kama Stamina, Roma Mkatoriki, Monny na wengine wengi, na moja kati ya nyimbo kubwa alofanya akiwa Tongwe ni Zimbabwe ya Roma Mkatoriki.

Geof Master alikua Producer mkubwa aliyetoa mchango wake kwenye kiwanda cha Muziki, japo alifanya kitu kwa ajiri ya Muziki, lakini mpaka anafariki, Muziki haukufanya kitu kwa ajiri yake.

Geof alifariki siku ya Ijumaa kwa matatizo ya Cancer ya Kichwa, Shukrani kwa Roma Mkatoriki, J Mulder CEO wa Tongwe Records ambao mlijitoa kujaribu kusaidia Matibabu ya Geof, ilifikia hatua Roma Mkatoriki akawa anafanya Mipango ya kumsafirisha Geof kwenda kutibiwa Marekani, Shukrani kwa mke wa Roma, Stamina, Fid Q, Monny, Banana Zoro, Madee, Producer Mr. T touch, Producer Bin Laden wa Tongwe na Wasanii na Producers wengine ambao jana Mlikuwepo kwenye Makaburi ya Wazo hil kumsindikiza mwenzenu.

Jana kuna kitu kikatuhuzunisha, Fid q akiwa MC alimpa nafasi Stamina atoe neno akiwakirisha Tongwe Records, na badaye akampa nafasi ya Upendeleo Msanii Monny toka Tongwe pia aseme neno (Huyu Monny ndo Msanii aliyekamatwa na Roma kipindi kile Roma ametekwa, coz walikua Studio wakifanya kazi na Marehemu Geof)
Monny anasema, kipindi hicho hakua na pesa hakua akimjua yeyote pale Tongwe Records, na akafika Studio akaomba kumuona Geof, baadaye akamwambia Geof yeye ni Msanii, ila hana pesa ya kulipa Studio, na alikua anatamani ku record, Geof aliamua kumsaidia aka record ngoma ya bure, japo alishindwa kuendelea akaanza kulia.........!

All in all maisha ya Geof Master yamefikisha mwisho na jana tukahitimisha safari yake.

Tunamshukuru Mungu kwa maisha ya Geof Master...!

Tangulia Manuva, Nenda Kingaru..... ... Tatizo la Hassan bado lipo pale pale....!

Mbele yetu, Nyuma yako.

R.I.P Geofrey Batista Msumule.
 
View attachment 2888320

Hassan ni.nani mkuu??? Sorry
 
Geof master salute
RIP
Ndio aliyeproduce wimbo wa Zimbabwe? Sidhani
Wengi huchanganya Kati ya beat composer na anayefanya mixing. Kuna muda anayefanya mixing ndio anaonekana kapiga beat hasa pale anapokua na jina kubwa kuliko anayepiga beat
Ndiye aliyefanya Beat, akafanya Mixing, pia aliimba Chorus na utaisikia pia Sauti yake mwishoni mwa Nyimbo...!
 
Hassan ni.nani mkuu??? Sorry
Tukikutana ama kuongea kwa Simu lazima angeanza kuuliza, Ndugu yangu vipi huko uliko, Hassan bado ni Tatizo...!?

Hassan = Pesa.

Kuna Noti ya Sh. 2,000 nadhani alikua anaipenda tu, na ile Noti vile ina Picha ya Rais mtaafu Ally Hassan Mwinyi, basi alizungumza Hassani akimaanisha Pesa, so ni kama angesema vipi upande wako kwa sasa Pesa bado ni Tatizo....!?

Kuna siku ananambia Brother, tumetoka kwenye Familia ambazo Hassan ni Tatizo, familia zinampenda Hassan ila Hassan anabagua Familia za kukaa, ni jukumu letu kumtafuta Hassan awe rafiki yetu, Hassan asiwe tatizo tena kwetu, ila awe rafiki yetu....!
 
R.I.P niliwah record ngoma kwake mwamba mtu poa sana, nilikuwa na k200 lakini mwamba akanitolea kitu bila malipo na ilisumbua sana ile ngoma East Africa dah pumzika salama nitaku wish sana
Mental illness patient
 
Habari wanaburudani, nimepokea taarifa za kusikitisha za msiba wa Producer Geof Master muda huu. Naambiwa alikua kalazwa Ocean road. Mara ya mwisho kuonana nae mitaa ya Tegeta alikuwa na uvimbe puani na alikuwa kwenye harakati za kufanyiwa upasuaji.

Naambiwa leo asubuhi amefariki. Mama yake anaishi Tegeta, naamini msiba wake pia utakuwa Tegeta. Kwa mlio mjini na mkaweza kufika msibani, tunaomba muendelee kutupa taarifa zaidi. Pumzika Pema Peponi Geof Master aka Manuva.

=======

Geof Master alisimamia wimbo maarufu wa 'Zimbabwe' wa Roma Mkatoliki pia alishirikishwa kwenye wimbo wa 'Ivan' na Roma Mkatoliki.

Geof Master ameacha watoto saba kutoka kwa mama wanne.
Huu ni mkwaju wake, Scooby ft Paul Son - usiku (mods iungeni na uzi)
 
Attachments

Back
Top Bottom