Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 5,383
- 18,776
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Mstaafu, Mussa Juma Assad, amesema "mazungumzo haya, 'unajua Jimboni kwangu barabara...', si mazungumzo ya bunge. Mazungumzo ya bunge ni policy (sera), ni utekelezwaji wa sera za serikali kwa ujumla."
Profesa Assad ametoa kauli hiyo akionyesha kusikitishwa kwake na kiwango cha mijadala inayofanyika bungeni kwa sasa, akisisitiza kuwa wabunge wengi wamejikita katika kudai mahitaji madogo madogo ya majimbo yao badala ya kusimamia na kuchambua kwa kina sera kuu za nchi.