Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 5,383
- 18,776
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Mstaafu, Prof. Mussa Juma Assad, amesema; "Mimi nafikiri tatizo letu kubwa ni tumeshindwa kutofautisha mijadala ya kisomi na siasa za nje. Wasiwasi wangu ni kwamba watu wanafikiri kwamba ukishakuwa na uongozi wa serikali ya wanafunzi ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, ambao yaelekea ni watu ambao wana mrengo ambao hauendani na sasa hivi mrengo wa serikali, wanakuwa wanatafsiriwa kama ni wapinzani. Na kwa namna hiyo limeathiri sana hilo nafikiri, yale mambo ya ubihishani wa kiakademia pale Chuoni Kikuu cha Dar es Salaam. Hilo moja."
"Lakini la pili ambalo mimi ninaliona ni mienendo ya walimu. Kwamba badala ya ku-encourage kukuza wanafunzi katika namna fulani, watu wanajihusisha zaidi katika kutafuta pesa nje ya chuo. Sasa ukishakuwa uko busy na vitu vyako vya pembeni, ukuzaji wa wanafunzi unakuwa unalegalega."