Prof. Assad: Wanaotaka viongozi wakubwa waongezewe madaraka ni 'mazuzu'

abulaaliyah77

JF-Expert Member
Joined
Oct 13, 2021
Posts
1,750
Reaction score
1,158
Huyu hapa Prof wa ukweli



PROFESA Mussa Assad, aliyewahi kuwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali ya Tanzania (CAG) amekerwa na viongozi wenye uwezo wa kuzungumza ukweli kwa maslahi ya Taifa kushindwa kufanya hivyo.

CAG huyo wa zamani amesema hayo leo Jumatano, tarehe 6 Oktoba 2021 jijini Dodoma, akizungumza katika mdahalo wa kuchambua Kitabu cha Rai ya Jenerali Ulimwengu na masuala ya Katiba, ulioandaliwa na Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC).

Katika mdahalo huo, Profesa Assad amempongeza Jenerali Ulimwengu kwa ujasiri wake wa kuandika na kuzungumza kile anachokiamini pasina woga wowote.

โ€œNimekuwa msomaji mzuri wa makala za Jenerali Ulimwengu na ni mtu tunaye mtazama kama hazina, kama kuna jambo la kusema atalisema, kwani kwa sasa kuna watu wamekuwa kama mazuzu.โ€

โ€œMtu amesoma sawasawa, anamwogopa mtu mwingine kwa sababu tu anatumia V8, nyumba ya serikali, anaogopa nikitoka hapa nitapata riziki wapi, mbona mimi nina miaka miwili nimeondolewa ofisini maisha yanaendelea,โ€ Profesa Assad

Leo Jumatano, Profesa Mussa ametimiza miaka 60 tangu alipozaliwa ambapo washiriki wa mdahalo huo, wamemwimbia wimbo maalum wa โ€˜Happy Birthday.โ€™

โ€œTunaishi siku moja, maisha yetu ni mafupi sana. Kila kunapokucha hakikisha unafanya vizuri sana kwani hakuna anayeijua kesho,โ€ amesema Profesa Mussa
 
Kumbe huyu ndiyo amewaita Mazuzu?
Nimeona Kubwa la Mazuzu linalaalamika kuitwa majina ambayo hawapendi, ila sikung'amua ni nani amewabatiza hilo jina.

Long live Prof Assad.

[emoji3][emoji3][emoji3]
Kwa hiyo sasa hiyo itakuwa official name yake?
Job Augustino Ndugai aka KUBWA LA MAZUZU!
 
Zuzu mkuu alichaguliwa na mazuzu 400,000๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚
 
Alichaguliwa na ombaomba 400,000 baada ya kuwahonga tisheti, kofia na wali.
Jamaa zuzu sana. Kongwa zaidi ya 50% ya wapiga kura wake ni masikini mazuzu wasiojitambua ndiyo maana wamekuwa wakimchagua kwa robo karne aendelee kuwatawala na yeye anajisifu kuwa anaakili kuliko hao mazuzu wenzake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreโ€ฆ