Prof. Assad: Wanaotaka viongozi wakubwa waongezewe madaraka ni 'mazuzu'

Prof. Assad: Wanaotaka viongozi wakubwa waongezewe madaraka ni 'mazuzu'

images - 2023-06-13T225856.148.jpeg
 
Kweli kabisa ni mazuzu yakazuzuka.wewe unaona kabisa mkataba ni tata lakini bunge zuzu linapitisha tu huo upuuzi
 
Habari ya mwaka juzi mnaleta kama ya Leo Ku push "agenda"??
 
Mazuzu=manyumbu hata yakiona yanaangamia yanaenda tu na kubaki kuchekana!
 
Huyu hapa Prof wa ukweli

View attachment 1985506

PROFESA Mussa Assad, aliyewahi kuwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali ya Tanzania (CAG) amekerwa na viongozi wenye uwezo wa kuzungumza ukweli kwa maslahi ya Taifa kushindwa kufanya hivyo.

CAG huyo wa zamani amesema hayo leo Jumatano, tarehe 6 Oktoba 2021 jijini Dodoma, akizungumza katika mdahalo wa kuchambua Kitabu cha Rai ya Jenerali Ulimwengu na masuala ya Katiba, ulioandaliwa na Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC).

Katika mdahalo huo, Profesa Assad amempongeza Jenerali Ulimwengu kwa ujasiri wake wa kuandika na kuzungumza kile anachokiamini pasina woga wowote.

“Nimekuwa msomaji mzuri wa makala za Jenerali Ulimwengu na ni mtu tunaye mtazama kama hazina, kama kuna jambo la kusema atalisema, kwani kwa sasa kuna watu wamekuwa kama mazuzu.”

“Mtu amesoma sawasawa, anamwogopa mtu mwingine kwa sababu tu anatumia V8, nyumba ya serikali, anaogopa nikitoka hapa nitapata riziki wapi, mbona mimi nina miaka miwili nimeondolewa ofisini maisha yanaendelea,” Profesa Assad

Leo Jumatano, Profesa Mussa ametimiza miaka 60 tangu alipozaliwa ambapo washiriki wa mdahalo huo, wamemwimbia wimbo maalum wa ‘Happy Birthday.’

“Tunaishi siku moja, maisha yetu ni mafupi sana. Kila kunapokucha hakikisha unafanya vizuri sana kwani hakuna anayeijua kesho,” amesema Profesa Mussa
Kazi kwao walinda legacy, Mzee wa Atake asitake and co.
 
Back
Top Bottom