Prof Bhalalusesa Kamishna wa Elimu tupe mikakati yako ya kuondoa kero za E lmu

Sigwame

Member
Joined
Dec 8, 2012
Posts
71
Reaction score
13
Wadau mtakumbuka mwezi Agosti. wakati wa bajeti ya Wizara ya Elimu Mh Waziri alimtambulisha kamishna mpya wa Wizara hiyo Prof Bhalalusesa, hivi huyu mama ameshaanza kazi rasmi na je katika hili la wadogo zetu kutaga mayai kwa wingi yeye anasemaje. Huu siyo wakati wa yeye kukaa kimya wakati elimu ya nchi hii iko mikonon mwake, Waziri ni Mwanasiasa tu! Ni wakati muafaka kwa yeye kufunguka tusikie sera zake
 
Huenda ameshaona maji marefu pale anavuta kwanza pumzi. Mmmh wizara ile, sijui????????
 
Ile wizara imejaa siasa tupu na kama ameshaanza kujiingiza kwenye siasa usitegemee ukombozi wa watanzania kielimu utoke kwake. Kimya kingi kina mshindo mkubwa tue na subira
 
I know prof. Bhalalusesa from days back, Alishawahi kuwa Dean wa FoED (Faculty of Education) pale Mlimani, sina wasiwasi na weledi wake ila tatizo la Tanzania yetu wanasiasa wamekuwa ndo kila kitu, hawawezi wakawaacha wataalamu wa fani mbalimbali wakatumia uwezo wao unless wanaendana na matakwa yao. Siasa kila kona ndo zimetufikisha hapa
 
Mama yule naye hakuna kitu, muoga sana kufanya maamuzi, kwanza kukubali cheo kile ni tamaa tu, kwani tayari ameshastaafu pale UDSM....
 
Mama yule naye hakuna kitu, muoga sana kufanya maamuzi, kwanza kukubali cheo kile ni tamaa tu, kwani tayari ameshastaafu pale UDSM....

Nakubaliana na wewe kabisa hata alipokuwa dean wa Shule Kuu ya Elimu hana alichokifanya maamuzi yote yalikuwa yanafanywa na Naibu Makamu Mkuu wa Huo Taaluma Prof Maboko. Kwa mantiki hiyo hapo atakuwa anacheza na santuri tu ya Kawambwa ni Prof asiyekuwa na independent thinking hata kidogo.
 
Mama yule naye hakuna kitu, muoga sana kufanya maamuzi, kwanza kukubali cheo kile ni tamaa tu, kwani tayari ameshastaafu pale UDSM....
Hapo hapana yuko kwenye secondment tu, bado hajafikia umri huo kabisa
 
jamani mama Prof Bhalalusesa ni mtu mweledi sana na namkumbuka zaid kama mwl wangu EA. Alipokuwa head wa department alisaidaia sana hii department ya Education planning and management na hata alipokuwa Dean wa faculty alionyesha kupevuka zaid kwani ndiye dean ambaye alisimamaia mabadiliko yenye tija kwenye kila department ndani ya faculty.

Tatizo ni kwamba UDSM iko na bureaucracy za kisiasa sana hivyo mama wa watu aliface challenge kubwa sana ili kuweza kuweka elimu iwe elimu na siasa iwe siasa na ndio mana alipigwa majungu sana. but dr Kitila mkumbo anakumbuka alivyojitahidi sana kumfanya huyu mama akubali challenge anazo face na pia kufanya nae kazi kwa karibu wakati wote wa uongozi wake.

kama ni kamishna wa elimu sina shaka na juhudi zake na uwezo wake katika planning and administration ila ninatatizo na uwezo na ujasiri wa yeye kukubali changamoto anazopitia katika kazi yake hii.

ukisoma professorial inaugural lecture yake utaona how capable she is kwenye hii kazi ila tu kiuhalisia atamudu changamoto?? to me ningeambiwa nimshauri ningesema amchukue Dr Kittila Mkumbo kama katibu wa wizara ya elimu ili wafanye kazi kwa pamoja.
 
Mkuu gfsonwin nafikiri hapo ni AE na sio EA
 
mmmh huyu Mama alikua Dean wa Faculty ya Education pale hajafanya chochote kile...sio Prof ni Associate Professor....kazi kweli kweli
 
mmmh huyu Mama alikua Dean wa Faculty ya Education pale hajafanya chochote kile...sio Prof ni Associate Professor....kazi kweli kweli

kwani mkuu ile professorial inaugural lecture hufanywa na watu gani??
 
tatz bongo sio mifumo jamani!mifumo ipo tu tn mizur na nina uhakika huyu mama hatoleta jipya zaidi coz siasa ndo imeshika hatam!kikwete cjui kapotelea wap jmn!
 
tatz bongo sio mifumo jamani!mifumo ipo tu tn mizur na nina uhakika huyu mama hatoleta jipya zaidi coz siasa ndo imeshika hatam!kikwete cjui kapotelea wap jmn!

Ni kweli hata wao wanadai kuwa mifumo ya elimu ipo mizuri, jana walikuwa kwenye TBC wakinadi sera zao na wakathibitishia umma kuwa mitaala ipo kwa hiyo kama kila kitu kipo tatizo ni nini Siasa au.....
 

Prof. gani hana independent mind? Basi siyo profesa by merit, au aliupata uprofesa kwa kigezo cha jinsia? Dhana ya 50/50 hadi kwenye taaluma.
 
mmmh huyu Mama alikua Dean wa Faculty ya Education pale hajafanya chochote kile...sio Prof ni Associate Professor....kazi kweli kweli

Tatizo la vyeo vya kupeana kwa jili ya kuhakikisha uwakilishi 50/50. Msihoji amefanya nini kwa sababu kwa hakika kuna kazi kubwa sana ambayoameshajiwekea legacy katika uongozi wake maana tangu tupate uhuru haijawahi kutokea wanafunzi waliofaulu kwa kupata 28% wakachaguliwa kwenda sekondari. Hakika huyu ana uwezo mkubwa kwa sababu katika kipindi kifupi alichokaa amefanya maamuzi mazito. Hakika ataondoa hii kero inayolisumbua taifa sasa hivi kwa kutoa waraka utakaosema waliopata D tatu waende A level. Stay tuned waraka utatoka hivi karibuni na kero itakwisha
 
Hahahahahahaha kweli nimeamini kuwa Kamishna wa Elimu ana uwezo mkubwa wa kufanya maamuzi magumu. Yeye ndiye mshauri wa waziri, alishauri Kidato cha I waende wenye alama 70 badala ya 100 out of 250. Baada ya kupata kigugumizi cha kuondoa kero ya kuandika waraka wa kuchukua watahiniwa wenye D tatu waende A level amekuja na mbinu kupitia kwenye kivuli cha Tume wa kushauri kubatilisha matokeo wakati suala la kubadili grade ranges lilitokana na Wizara yenyewe.

Badala ya kufanya kazi anaona watu wote pale wizarani hawajasoma na ana dharau sana na majibuno, anapenda kujipambanua "mie ndiyo Kamishna w Elimu, inabidi kila kitu moitishe kwangu mniombe ruhusa mkitoka mie ndio kamishna" Sawa inaeleweka wewe ni Kamishna lakini tuambie umma ukamishna wako unasaidiaje kuleta tija katika elimu. Uchakachuaji umeshamiri katika kipindi kifupi cha Kamishna huyu ambaye hajamaliza hata mwaka. Sasa akimaliza miaka angalau miwili tu elimu itabaki kitu au hata anayetaga mayai ataenda A level ili kujaza madarasa?

RIP wanafunzi waliojiua kutokana na wizara kutokuwa na dira na miongozo kiasi ambacho baraza linaenda hata haijulikani nini kinafanyika
 
Huyo ni mchumia tumbo tu anawapelekesha Mkurugenzi wa Sekondari na Msingi halafu wannampoza kwa vibahasha. Anapenda sana kuvuta bahasha
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…