Prof. Florens Luoga: Crypto-currencies are not safe as far as we know

Sasa muggyen tunaongea haikuwa haki kumdhihaki prof.

Uzuri kuna aina Tofauti za wawekezaji I read Warren Buffets book that guy is afraid of losing. Yeye mwenyewe alikiri mwanzoni wakati anaanza kufanyabiashara hakuwahi kununua hisa za kampuni kubwa.

He scavenged the dying ones na akaziongezea thamani. He believed the less he invested The less he will lose such a risk averse.
 

Sasa nakuuliza tena. Unijibu.

1. Kwa sababu umesema elsavado wana account ya bitcoin basi wana speculate Je nao BoT kwa sababu wana account ya fedha za ndani na nje nao wanaspeculate?
El Salvador wanaspeculate Hilo halina ubishi na ndio maana baada ya thamani ilivyopanda wakauza bitcoin 20 na faida kuitumia kuitumia kujenga shule. Hakuna siku imetokea BoT wameuza Dola pale ambapo TZS imepanda ili wapate faida kama el Salvador wanavyofanya.

Hata Rais amesema kuwa faida watakayokuwa wanaipata baada ya kuuza bitcoin itapelekwa kwenye shughuli za jamii
Kwa nini unauliza swali halafu hutaki kujibu swali! Basi sawa.
Forex reserve ya Tz ni Dola Kwa kiasi kikubwa na hakuna Dola ambayo benki kuu wanatumia kununua sarafu nyingine halafu wahifadhi zote zinapatikana baada ya BOP,

El Salvador wanaacha "fursa" kupunguza Makali ya mdororo WA uchumi wao hivyo mi niliona walipaswa wannunue bitcoins Kwa kiasi kikubwa.
Kwa kuwa bukele anatarajia bitcoin itakuza GDP Kwa 25%.

Sasa basi, kwa nini hiyo el salvador hawakutumia forex reserve yao yote ya dola(bil 2 kufikia april) kununua bitcoin? isipokuwa ni kasehemu kadogo ya reserve.
 
Mkuu unatakiwa uzinduke, duniani sio china tu!View attachment 2024796
Huyu ni kilaza Tu kama vilaza wengine , ni kweli crypto_Currency inaweza kuwa inafanya vizur , ni aibu Kwa Taifa kuliingiza kwenye mfumo wa Bahati nasibu ambao hauko verified kisheria ..!! Japo Kwa sasa anaweza kuonekana mjanja , Likitokea la kutokea wote yeye na wenzake wataonekana mafala ...!!
 
Uchumi wa kubet [emoji125][emoji125][emoji125]
 

Jibu la swali lako ungepata kama ungejibu swali langu ila kwa kukusaidia ni kwamba kilanchi tofauti na shilingi yao pia wana reserve ya shilingi za kigeni. Vivyo hivyo hata elsavador nao wenda hawakutumia reserve yao yote ya usd ili wawe na usd katika reserve yao (ofcourse pamoja shilingi za mataifa mengine).

Hilo limeisha ...

Lakini mkuu kwa mantiki unayo isemea basi kila nchi ina speculate maana hata Tz yenyewe ina ina milikumi hisa za makampuni mbali mbali mfano serikali ya Tz ina miliki hisa kuanzia crdb, nmb, airtel nk nk nk!

Na kila mwaka huwa wanapewa gawio na kuna mwaka magu akaenda mbali zaidi kulazimisha makampuni walete gawio!

Sasa kama Elsavador wanatumia faida ya bitcoin kujenga miundo mbinu ya kijamii kwenye nchi yao unasema wana speculate je Tz inapotumia gawio la makambuni kujenga miundo mbinu ni sahihi tukisema serikali ya Tz nayo ina speculate?
 
Unasema limeisha Kwa kutoa jibu ambano huna uhakika nalo.
Unafananisha share za serikali zilizowekezwa kwenye (real economy) yaani uuzaji WA bidhaa na huduma na uwekezaji WA kwenye bitcoin. Shea zinawakilisha umiliki WA shirika ambapo wamiliki mwisho WA mwaka hugawana faida ama hasara.

Great depression ya USA ilisababishwa na speculations kwenye hisa, serikali ya Tz hainunui na kuuza hisa Bali hisa inazimiliki kama moja uwekezaji katika shughuli za UZALISHAJI NA UTOAJI UHUDUMA WA hayo makampuni (mashirika).

Mzee au unachukulia CRYPTOCURRENCY kuwa ni bidhaa?
 
Umeishia kujizunguka mwenyewe! Cha msingi ni kwamba umekubali kwamba hata serikali ya Tz nayo itakua ina speculate kama unasema elsavador wana speculate. Hilo ni jambo jema..

Cryptocurrencies ni service na pia bidhaa kama ifwatavyo..

Ni service kwa muktadha wa DeFi au decentralized finance. Kwa hata wewe uliyepo hapo chato unaweza kopa hela instantly bila mbwembwe za shahidi wala wakili!

Ni bidhaa kwa muktadha wa NFT's na gaming tokens! Kama ni mfwatiliaji mzuri wa crypto world basi hapa sina haja kuandika zaidi!
 
Mkuu lumanyisa sijamdhihaki Gavana wetu na siwezi kufanya ivo, amenizidi mbali sanaaa ni kama kusema ni mzee wangu.

Kwa nafasi yake kama Gavana kweli ana haki ya kuwa conservative. Kauli yake inatosha kumbebesha zigo la lawama siku mambo yakiharibika, ila kwa wanao/tunao elewa biashara hii, crypto ni good investment, sababu ina volatility ya kutosha. Volatility ndio faida inapopatikana.

Mfano hapo zamani kidogo nliwahi kununua hisa DSE kwa lengo la kuhold 3-5 years lakini nliziuza baada ya kuona very low volatility. Hio akili nlvopeleka kwenye crypto imenifikisha mahali.

Mfano ni huu hapa, nlichukua XRP (Ripple) 10000 kwa price ya $0.03, hivyo nikawa nimetumia $300 na leo hii Ripple inauzwa at $0.9 so kwa hesabu ya haraka investment yangu imekuwa na kuwa thamani ya $9000 (sijamaliza hata 5 years). Kumbuka mie nimeweka $300, so nikauza nusu ya investment kuongeza mtaji ($4500) na iliobaki naweza kuhold hadi for 10+ years sababu pesa nlioweka nishatoa na faida juu.

Sasa mie ningekuwa governor cha kuongeza tu, ningewahimiza vijana na watu wote wenye vipato kujifunza dunia inapokwenda na kwenda nayo sambamba ila tu jambo la msingi. Jua tu hii ni speculation.

Kama tunaweza fundishana jinsi ya kuwekeza kwenye soko la hisa, kweli tutashindwa kufundishana kwenye hili?! Fikiria kijana apata mtaji wa $9000 (mil. 20.7 TZS) mbona tayari kaipunguzia serikali mzigo wa unemployment na pengine tayari anaweza kutoa ajira kwa vijana wengine. Na hii pesa sio virtual economy ikija hapa inakuwa taxed kupitia VAT na bado inakuza uchumi wa ndani.

Ushauri wangu, ni badala ya serikali kuwa conservative na mabadiliko yoyote ya teknologia yanapotokea ni bora kuwa adaptive. Hio itasaidia kufungua fursa kwa vijana na jamii kwa ujumla. Kwa ongezeko la watu, soko la ajira la ndani haliwezi kutukidhi wote, yangu ni hayo tu.
 
Shida utapeli

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…