Prof. Issa Shivji bado tunahitaji Tanganyika huru

Imma Saro

JF-Expert Member
Joined
Dec 19, 2012
Posts
394
Reaction score
197
Usomi wamtu yoyote yule dunia hueshimiwa na pia usomi wake upuuzwa na kuonekana ujinga haya yote msomi anaweza kuyataka mwenyemwe.

Inashangaza Shvji ambye alikuwa na msimamo na alitamka mwenyewe kuhusiana na Mabadiliko ya katiba ya Zanzibar mwaka 2010 kuwa yamevunja katiba ya JMT leo amegeuka nakusema mabadiliko hayo hayajavunja katiba ya JMT.

Shivji unaenda mbali zaidi pale anaposema kuwa serikali tatu zitavunja muungano.

Shivji anakwenda mbali zaidi na kusema Zanzibar kuwa na bendera na nyimbo sio kosa.

Msomi huyu anafananisha mashirika ya nje kuwa na bendera na nyimbo zao huku ni kukosa uwelewa wa haya mambo.
Shivji anakwenda mbali akisema Zanzibar hawana makosa.

Tunafahamu Zanzibar hawana makosa wenye makosa ni serekali ilioruhusu kuvunja katiba.

Kumbuka haya Prof Shivji
Kama Zanzibar wana nyimbo na bendera yao basi na sisi Tanganyika,
1. Tunahitaji Nyimbo na Bendera,
2. Tunahitaji Katiba ya Tanganyika Kama ilivyo ya Zanzibar
3. Tunahitaji Bunge letu lisilo wahusisha wazanzibari,
4. Tunahitaji vikosi vya ulizi kama Zanzibar,
5. Tunahitaji Rais na Makamu wetu kama Zanzibar
6. Tunahitaji mamlaka kamili kama Zanzibar,
7. Tunahitaji kujua bajeti ya Tanganyika yetu,
8. Tunahitaji Vyuo vikuu vya Tanganyika,
9. Tunahitaji haya yote kwa kuwa wezetu wanayo kwani leo sisi mtufiche kwa mwavuli wa muungano.

Ikiwa Tanzania ni Muungano wa Tanganyika na Zanzibar basi neno Tanganyika liko wapi?

Hitimisho;
Napenda muungano Wenye Usawa pande zote za Muungano,Wenye kutuleta pamoja kama Taifa Huru lenye kuheshimu uhuru wa upande mwingine;

Prof Shvji na elewa wajua watanganyika tumenyanyaswa bila kujijua, ukoloni ndani ya nchi ni hatari;
 
Prof. Shivji akosoa rasimu ya katiba, asema muundo wa serikali 3 utavunja muungano, asema katiba ya Zanzibar haina makosa yoyote,shivji amesema hayo leo kwenye kongamano la vyuo vikuu kuhusu muungano lilorushwa live na TBC1 je matamshi haya ya prof Shivji ni ya kizalendo?au ni ya kisiasa kama yale ya JK kwenye kufungua bunge la katiba?
 
...its nod coincidency mkutano wa jana na huo wa shivji,alipokuwa na mawazo huru alikuwa anaongea kweli lakini sasa naamini amekuja kimkakati baada ya kufundwa na ikulu na kuinunua reputation yake kwa maslahi yao binafsi,ni aibu kwa msomi kama huyu....
 
Hivi huyu Prof. ni Mzanzibar au Mtanganyika? Mbona alikuwa akiitetea sana Zanzibar huku akiwa kama anajipendekeza kwa JK? Ni mawazo yangu tu
 
Ni mawazo yake pia ambayo alistahili kuyatoa wakati wa mchakato wa katiba mpya ambapo kila mdau alikuwa na uhuru wa kusema alichoona kinafaa kusema period. Warioba alikuwa mkuu wa jopo tu wala hakupendekeza serikali tatu hivyo ni kosa kumbebesha lawama baba wa watu!
 
Msimamo wa Prof. Shivji unabadilika kila wakati kulingana na mazingira. Alafu anaitetea sana Zanzibar. Hivi niulize kitu. Je tukiingia kwenye shirikisho la Africa Mashariki (East African Federation) kutakuwepo na serikali ngapi? Je serikali ya shirikisho hilo itakuwa na raslimali au la au raslimali zitabakia za nchi shiriki?
 
Yote sawa tu, ni maoni yake. Hata warioba alitoa maoni.
 

Huyo naye ni mnafiki tu anatumiwa kisiasa!
 
Hivi huyu Prof. ni Mzanzibar au Mtanganyika? Mbona alikuwa akiitetea sana Zanzibar huku akiwa kama anajipendekeza kwa JK? Ni mawazo yangu tu

Ni mipango maalum imepangwa ili kuunga mkono hotuba ya rais jakaya na kumpotosha j.warioba ili ionekane serikali 3 kumbe haina maana., kama shivji alikuwa na cha kusema juu ya rasimu 2 ya katiba ilikuwa pale mapema tu lakini ni mipango ya kulishizwa maneno na ajenda zao tu ccm, taaluma yk shivji haikumsaidia saivi ameonekana wazi ni mtu wa kupotosha na ameshadharaulika tayari, kule Zanzibar tunamjuwa vyema sn
 
Ukweli daima unauma sana shivji kasema kweli tena kweli iliyokali.
 
kumbe Shivji wa Kilosa?! Kwa hiyo anatumika kisiasa? Nilivosikia tbc ndo wanarusha nilistuka sana, ila sasa ni kama nimeelewa ni kwa nini.
 
Shivji kazungumza ukweli mtupu shida ya warioba alikuwa anapotosha akidhani hakuna watu wanaojua haya mambo sasa anazidi kuzodolewa.
 
Imma Saro wewe ndio prof kwa mawazo yako murua ila shivji sidhani kama anastahili kuitwa profesax
 
kumbe Shivji wa Kilosa?! Kwa hiyo anatumika kisiasa? Nilivosikia tbc ndo wanarusha nilistuka sana, ila sasa ni kama nimeelewa ni kwa nini.
Huko ni kuchanganyikiwa mkuu hayo mawazo potofu kabisa kabisa.
 
kumbe Shivji wa Kilosa?! Kwa hiyo anatumika kisiasa? Nilivosikia tbc ndo wanarusha nilistuka sana, ila sasa ni kama nimeelewa ni kwa nini.

Hata mimi ni mmoja wa watu ninaoamini sasa shivji katumika kama wa kundi 210 huyu mzee amekuwa sio mkweli anapoongelea swala la kitaifa na hii ni dhambi itakayo kula wana taaluma wa nchi hii vizazi kwa vizazi mpaka siku ya ukombozi wa kweli
 

Mkuu.
Halikuwa Kongamano la vyuo vikuu.
Rather lilikuwa kongamano la wachumia tumbo lililoratibiwa na CCM na kupigiwa chapuo na akina Pasco
 
Last edited by a moderator:
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…