Prof.J, hatasahaulika kamwe na wimbo wake wa J.O.S.E.P.H

figganigga

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2010
Posts
25,724
Reaction score
55,906
Mwaka 2006 ndio ilitoka album ya tatu ya Prof Jay ambayo inafahamika kwa jina la J.O.S.E.P.H. Lakini J.O.S.E.P.H ni wimbo ambao uliweza kulichaguliwa kuwa wimbo bora wa Bongo Fleva/Hiphop BBC na Radio One Awards
Ila JOSEPH ni jina lake ambalo aliamua kuleta ubunifu ili aweze kufikisha ujumbe stahiki kwa jamii ya wapenda muziki.

Maana ya JOSEPH kwa jinsi yake alivyochambua ilikuwa ni J ilisimama kama JIFUNZE, O imesimama kama ONA, S ikasimama kama SEMA, E ikasimama kama ELIMIKA,🙂P ikasimama kama PITIA na H ikasimama kama HAMASIKA.

Ubunifu kama huu umekosekana katika muziki wetu, bali watangazaji wamekuwa wakisifu zaid mahusiano ya fulani na fulani, kusenngenya na mengine ambayo kimsimgi hayajengi muziki wala kuelimisha jamii!!
Licha ya watu kuburudika ila muziki ni moja kati ya njia chache za kuelimishana.

NI vyema wadau na watangazaji wazingatie hilo.
Team tizneez tunatambua na kuheshimu mchango wa Prof Jay katika muziki wa kizazi kipya!!
 
Hizo ndizo zilikuwa nyimbo za maana nyimbo kama J.o.s.e.p.h,ni msanii gani wa leo hii anaweza kuandika mashairi makali kama yale zaidi ya leo tu matakataka yamejaa kwenye media na mastory ambayo yapo kabisa kinyume na maadili ya kisanii.
 
Mida flani nilikiwa nasikiza ngoma za Nature za kipindi hicho daaah yani kama zimetoka jana unasikiliza nyimbo una feel.
 
Sauti ya geto inayokuja na vina vyenye maana nyepesi
Hili ni neno turudi kwake lord of mercy
 
Mwaka 2006 ndio ilitoka album ya tatu ya Prof Jay ambayo inafahamika kwa jina la J.O.S.E.P.H. Lakini J.O.S.E.P.H ni wimbo ambao uliweza kulichaguliwa kuwa wimbo bora wa Bongo Fleva/Hiphop BBC na Radio One Awards
Ila JOSEPH ni jina lake ambalo aliamua kuleta ubunifu ili aweze kufikisha ujumbe stahiki kwa jamii ya wapenda muziki.

Maana ya JOSEPH kwa jinsi yake alivyochambua ilikuwa ni J ilisimama kama JIFUNZE, O imesimama kama ONA, S ikasimama kama SEMA, E ikasimama kama ELIMIKA,🙂P ikasimama kama PITIA na H ikasimama kama HAMASIKA.

Ubunifu kama huu umekosekana katika muziki wetu, bali watangazaji wamekuwa wakisifu zaid mahusiano ya fulani na fulani, kusenngenya na mengine ambayo kimsimgi hayajengi muziki wala kuelimisha jamii!!
Licha ya watu kuburudika ila muziki ni moja kati ya njia chache za kuelimishana.

NI vyema wadau na watangazaji wazingatie hilo.
Team tizneez tunatambua na kuheshimu mchango wa Prof Jay katika muziki wa kizazi kipya!!
Mkuu hii nyimbo nimeitafuta kwa udi na uvumba kwa muda mrefu cjaupata tafadhar nomba unisidie natanguliza shukran
 
Nakumbuka chorous alisimama rama de daaa hii nyimbo ni balaa kuanzia beat na kila kitu
 
Miaka 10 nyuma ila ngoma kama imetoka jana vile aiseee
 
Kitambo sana, kipnd kile bongo Flava ulikuwa mziki kweli kweli, mashairi na ubunifu katika kazi zao ndio ilikua nguzo ya kumweka msanii kwenye chati!! Ninakumbuka tulikuwa na album ya J.O.S.E.P.H na zile mbili za mwanzo.
 
Km mtu anayo aitupie humu,au japo link..natanguliza shukrani
 
Back
Top Bottom