Prof. Kabudi ahudhuria hafla ya uzinduzi ripoti ya BBI nchini Kenya inayopendekeza uwepo wa cheo cha Waziri Mkuu na Kiongozi wa Upinzani Bungeni

Prof. Kabudi ahudhuria hafla ya uzinduzi ripoti ya BBI nchini Kenya inayopendekeza uwepo wa cheo cha Waziri Mkuu na Kiongozi wa Upinzani Bungeni

johnthebaptist

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2014
Posts
97,869
Reaction score
171,716
Waziri wa mambo ya nje Prof. Kabudi amehudhuria hafla ya uzinduzi wa ripoti ya Building Bridge Initiatives (BBI) nchini Kenya ambayo imehudhuriwa na viongozi wote wakuu wa Jamhuri ya Kenya.

Miongoni mwa mapendekezo ya BBI ni haya:

1. Uwepo wa cheo cha Waziri mkuu ambaye ni lazima awe Mbunge wa kuchaguliwa na atalipwa mshahara wa mbunge

2. Uwepo wa Baraza la Mawaziri ambao watatokana na wabunge na watalipwa mshahara wa mbunge.

3. Uwepo wa Kiongozi wa Upinzani Bungeni (KUB) ambaye atakuwa ni yule aliyegombea urais na kuwa wa pili, ataingia bungeni kama mbunge na ataunda baraza la mawaziri kivuli

4. Watumishi wa umma hawataruhusiwa kufanya biashara na serikali.

Na mengine mengi.

Chanzo: Citizen Tv

Zaidi Tazama hapa:








Pia soma
 
Inasemekana kwamba uboreshaji wa mji wa Nairobi kwa kujenga miundombinu na flyovers waliuchukua baada ya Dar es Salaam kuuanzisha lakini tukabakia tu na maenno wenyewe wakatekeleza na sasa hivi wako mbali.

Sasa angalia, tulianzisha demokrasia bora na imara na kwa 'uslow' wetu tunaiua na wenyewe wanaitekeleza. Mwezi jana tu na spika aliende (eti) kujifunza uonyeshaji bunge live wakati huo huo pakiwa na mashaka kama bado pana bunge pande hii!
 
November 27, 2019
Nairobi, Kenya

Tanzania and Suriname pledged their support for Kenya's bid for a non-permanent seat on the UN Security Council

Tanzania’s Foreign Affairs Minister Palamagamba Kabudi and the President of Suriname Desire Delano Bouterse delivered the assurances to President Uhuru Kenyatta at State House, Nairobi.

Mr Kabudi who paid President Uhuru a courtesy visit as a special envoy of President John Pombe Magufuli, said Tanzania has full confidence in the ability of Kenya to represent the African continent in the security council.

“We have confidence in Kenya, that you will champion the African voice and will strongly advocate the continent’s position in the UN body,” Mr Kabudi said.

The special envoy, who was accompanied by Tanzania’s ambassador to Kenya Dr Batilda Salha Buriani, acknowledged Kenya’s leading role in the push for a united and progressive Africa.

On the maritime border dispute with Somalia, the special envoy said Tanzania supports Kenya's stand on the need to pursue the option of an out of court settlement.
Source: Tanzania, Suriname back Kenya’s bid for UN Security Council seat | The Presidency
www.standardmedia.co.ke

Earlier on :

7 Nov 2019
Kenya begins his bid for a non-permanent seat in the UN security council


Source: Kenya CitizenTV
 
Watanzania wenzangu, hebu angalieni mchakato wa BBI katika Citizen Tv live ya Kenya. Unahusu Katiba ya Kenya. Mchakato huu una manufaa pia kwa Tanzania kwa baadhi ya mambo kwani kuna vitu vya kujifunza na kuiga.

Tanzania inawakilishwa na Mh. Kabudi, Waziri wetu wa Mambo ya Nje.
 
Inasemekana kwamba uboreshaji wa mji wa Nairobi kwa kujenga miundombinu na flyovers waliuchukua baada ya Dar es Salaam kuuanzisha lakini tukabakia tu na maenno wenyewe wakatekeleza na sasa hivi wako mbali.
Vipaumbele vya jiji la Dar havikuwa kujenga flyovers bali kutafuta suluhu ya kupunguza foleni jijini. Na katika upembuzi yakinifu uliofanywa na serikali ya Mkapa 2003 ikaonekana daladala ndiyo chanzo cha foleni hivyo ikapendekezwa kuanzishwa usafiri wa umma. Treni za jijini zilionekana kuwa na gharama kubwa na hivyo BRT ikachaguliwa.
Sasa angalia, tulianzisha demokrasia bora na imara na kwa 'uslow' wetu tunaiua na wenyewe wanaitekeleza.
Tanzania bado ina demokrasia bora Afrika, marais wote watano wametoka makabila tofauti tofauti, ni nchi gani nyingine Afrika imefanya hivyo?
Mwezi jana tu na spika aliende (eti) kujifunza uonyeshaji bunge live wakati huo huo pakiwa na mashaka kama bado pana bunge pande hii!
Umeandika kinyume, Ndugai alienda bunge la Kenya kuwafundisha jinsi ya kuliendesha kwa kiswahili.
 
HOTUBA NZIMA YA PROF. KABUDI
Palamagamba Kabudi hata Tanzania chini ya CCM ina matatizo hayo hayo ya ujomba, ukabila , ufisadi na ubaguzi wa kiitikadi za kisiasa. Lini CCM itakuja na BBI (Building Bridges Initiative) baada ya kuvuruga nchi ya Tanzania kupitia 'uchaguzi' haramu wa serikali za Mitaa na vijiji.
 
Muhimu hapo sio Kiswahili alichozungumza, muhimu ni hayo alitosema, wakenya wengi inaonekana wamechoshwa sana na " Division & tribalism"
 
Amekitendea haki kiswahili, nimependa hii hotuba yake
 
Back
Top Bottom