Prof. Kabudi ahudhuria hafla ya uzinduzi ripoti ya BBI nchini Kenya inayopendekeza uwepo wa cheo cha Waziri Mkuu na Kiongozi wa Upinzani Bungeni

Prof. Kabudi ahudhuria hafla ya uzinduzi ripoti ya BBI nchini Kenya inayopendekeza uwepo wa cheo cha Waziri Mkuu na Kiongozi wa Upinzani Bungeni

Hehehe ila huyu jamaa huwa napenda kumfuatlia, siku mtampa urais ndio nitaanza kuwaskliza nyie watu maana ni kichwa sana.

Tatizo amenyang'anywa ndege akiangalia tu, alikuwa akionywa kuhusu mkulima lakini anapuuza.
Na pia akirudi kwao awafundishe CCM kuzingatia haya haya ameyasema na kutuasa, maana nyumbani kwao huko Tanzania CCM imeharibu nchi ikavurugika, hamna demokrasia wameendekeza full ubaguzi.
 
Kawachamba halafu kawashikisha Serikali na Bunge zima mikono na kuwaapisha huku wakijikuta wanasimama wenyeweer! Prof. Kabudi ni noma...
Umewaona wale viongozi wakuu pale jukwaani, wamekaa wamelowa utafikiri wanafungishwa ndoa na padri.
Aliyowaambia wakiyafuata kenya itasonga mbele sana katika ukanda huu.
''Kenya is the economic engine of East Africa.''- Prof. Kabudi.Sijui kama mmesikia na hiyo pia? Sasa kwasababu msomi wenu na baba yenu ameyasema hayo, hamna budi ila kukoma kabisa kukesha kwenye jukwaa hili mkitema mipovu na kutanua misuli yenu ya utapiamlo.
 
Aa wapi hajamaanisha ile ya GDP ya $99 bln bali ya less than $75 bln!
 
Aa wapi hajamaanisha ile ya GDP ya $99 bln bali ya less than $75 bln!
Tanzania mmefikia hata hiyo $75 bln, achilia mbali GDP ya Kenya ya $99bln? Narudia tena, ''Kenya is the ECONOMIC ENGINE of East Africa''. Sio maneno yangu, ni ya Kabudi, ambaye ulikuwa unamshabikia dakika chache zilizopita ukisema kwamba amewachamba wakenya. 😀
 
Huyo Kabudi kuna vitu amevisema nikaona kama atakua anatuma ujumbe fulani kwa CCM na mkulu wenu japo kaifanya kama vile anaambia Wakenya, haswa sifa alizomumiminia rais Uhuru, kuna vijimaneno katumia humo nikaona ni kama message sent ila address ya maagogoni Tanzania.
 
Mimi nasubiri 2022 Uchaguzi ujao nchini Kenya, niliwaambia rafiki zangu kwamba haya yote ni maigizo ya kutafutiana madaraka kwa mlango wa nyuma hawaniamini, wanawaamini Wanasiasa wao, sasa subiri watu waikose Ikulu 2022 halafu uone jinsi watakavyoikataa tena hiyo BBI, watarudi tena na mpango mpya, au wataingia barabarani.

Nilichokiona Kenya 90% show, 10% real!
 
Yani leo Tanzania nzima ilikuwa inatazama televisheni za Kenya? Duuuuh!
 
MK254,
Hahah next president ni Majaliwa,
Sijui kama umekosea spelling ya jina yake,if not wrong ni prime minister
 
Hujaeleweka ulichoongea. maana mada iliyoko mezani ni BBI - Kenya.
Nimemnukuu Kabudi, mada iliyopo mezani ni kuhusu hotuba yake. Hujaitizama hiyo video, sanasana hapo aliposema kwamba Kenya is the economic engine of East Africa?
 
What was the theme of that gethering? usilete ubishi wa kitoto. 😛 😛 😛
Ina maana hajaona na kusikia mada za msingi Kabudi alizozizungumza au hiyo kwake ndio kitu cha maana, hawa jamaa wana akili fupi mnoo 😂😂😂
 
What was the theme of that gethering? usilete ubishi wa kitoto. 😛 😛 😛
Mimi nimemnukuu tu. Ubishi wa kitoto ni kama huu hapa chini, wa kuingiza hadithi za ndoa na padre kwenye 'gethering' ya kujadili mambo ya maana.
Umewaona wale viongozi wakuu pale jukwaani, wamekaa wamelowa utafikiri wanafungishwa ndoa na padri.
Aliyowaambia wakiyafuata kenya itasonga mbele sana katika ukanda huu.
 
Nimesikiliza na kuona Citizen Tv ya Kenya wameonyesha speech ya kinafiki ya Prof. Kabudi.

Kisha wakawahoji wananchi wa kenya kuhusi mambo ambayo Prof Jalalani ameongea huko.

Kwanza wamemwona ni mnafiki mkubwa kwa kuikandia Kenya kwamba ina ina matatizo ya kisiasa wakati kiuhalisia Tanzania ndio ina matatizo makubwa hasa kwa kukosa demokrasia.

Pia wameonyesha kukerwa na kauli yake alipowashauri wakenya waachane na siasa na malumbano na wafanye siasa za maendeleo kama Tanzania inavyofanya kana kwamba ni jambo zuri wakati wakenya wanajua watanzania waliokimbia nchi kwa sababu za kisiasa.

Pia wanasema hana moral authority ya kuishauri Kenya kwenye demokrasia wakati nchi yake wananchi hawapo huru kuongea.

Kiukweli nimejisikia vibaya sana kwa jinsi Wakenya wanavyotuona watanzania tulivyo wanafiki na wapumbavu.

Binafsi kama Mtanzania nawapongeza sana Wakenya kwa hatua wanazochukua hasa Rais Kenyatta.

Tanzania kufikia hatua ya Kenya bado ni ndoto, kwa namna hiyoKenya itaendelea kuwa super power wa East Africa.

Mungu mbariki Kenyatta na maombi yangu hii roho nzuri imuingie na Meko wetu.
 
Back
Top Bottom