Prof. Kabudi ahudhuria hafla ya uzinduzi ripoti ya BBI nchini Kenya inayopendekeza uwepo wa cheo cha Waziri Mkuu na Kiongozi wa Upinzani Bungeni

Prof. Kabudi ahudhuria hafla ya uzinduzi ripoti ya BBI nchini Kenya inayopendekeza uwepo wa cheo cha Waziri Mkuu na Kiongozi wa Upinzani Bungeni

Kongole sana Prof. Kabudi umetuwakilisha vema kwa hekima na maarifa Watanzania.Hotuba halisia,ya udugu,elimishi na kubwa zaidi moral umewafa nyisha agano jema ni sals kwa Mungu.
 
Ukweli ni kwamba kabudi ni mnafiki. Anaongea Kenya kana kwamba Tanzania ni nchi ya demokrasia wakaTi hali tuliyofikia ni zaidi ya burundi
Toka jana unatembea na haka ka kipande tu. Ina maana wakenya wote walitoa maoni ni hako ka kipande tu?

Aibu nyingine mnajitakia tu aisee
 
Nilimsikiliza jana. Naamini ndio atakuja kuvaa viatu huko magogoni. He's strong, ana points na anajiamini mbaya!
 
Nilimsikiliza jana. Naamini ndo atakuja kuvaa viatu huko magogoni. He's strong, ana points na anajiamini mbaya!
Unachosema ni sahihi kabudi yuko vzr na hata wakenya wengi wamempingeza tatizo baadhi yetu humu chuki za ki vyama zinatutoa ufahamu
 
Kabudi aside, sikumsikiliza ila najua hamna lolote la maana aliloongea. Nataka kusema tu, kuna wanasiasa wakenya ni wapumbavu sana, nchi ina katiba nzuri iliyopiganiwa kwa miaka mingi leo wanataka waivuruge kwa maslahi binafsi, eti BBI.

Tatizo la Kenya ni wizi wa kura na ukabila uliopitiliza,hizi ndio root causes za vurugu. Sasa haya majinga yanafikiri suluhisho ni kuweka nafasi ya waziri mkuu atayegawana madaraka na rais, sijui KUB pia atakuwepo na blah blah nyingine.

Yanalazimisha kuchanganya presidential system na ile parliamentary system ya nchi kama UK or Israel. Yaani haya mambwiga yanalazimisha kuwa na hybrid system eti ili kwenye uchaguzi mkuu the winner should not take it all, eti kabila moja isichukue kila kitu.
Eti kuna watu humu wanasifia huu upuuzi. Mimi sio expert wa constitutional law, lakini sisi tupo kama hatujitambui,kusifia sifia tu. Ndio maana tuna katiba mbaya, tuna resemblance ya presidential system halafu eti tukalazimisha kuwa na waziri mkuu ambaye hana madaraka yoyote ya maana,ni kiranja tu wa cabinet, huwa pia namuona anapuyanga tu mikoani kutoa maagizo na matamko.
 
Kilatha,
Kwa wapinzani 'kususia' au 'kutosusia' sasa hivi hakuna tofauti yoyote maana matokeo yanabaki kuwa vilevile yalivyopangwa na CCM. Bila shaka linalotegemewa ni hilo unalolieleza hapa, wapinzani wasusie uchaguzi mwakani; lakini hata kama hawatasusia matokeo ya uchaguzi hayo hayana shaka.

Ni jambo la kustaajabisha kwa mtu kudhani kwa hali ilivyo sasa Tanzania ni tofauti na hali ilivyo katika nchi hizo tatu
 
Mawaziri kuwa wabunge mimi sijalikubali huko ni kurudi nyuma na sio kwenda mbele.
ndio mwanzo wa serekali kuteka Bunge. mwisho wasiku wabunge badala ya kuisimamia serekali wanajikuta wanaitetea kisa tu wanjiona sehemu ya serekali.
 
Kalamu1,
Aina maana CCM iachiwe kushinda kirahisi kama ilivyotokea kwenye huu uchaguzi wa serikari za mitaa halafu watu waanze kulia kulia kwa maamuzi yao wenyewe.
 
MK254,
Hizo zilikuwa dili za watu, mkulima ni kisingizio tuu, ndiyo maana Magu aliamua kuacha kulipa. Wewe unafikiri pesa za kufanya miradi yote hii anayoifanya zinatoka wapi?

Jamaa amekata mirija mingi ya wizi, watu wanahasira nae, wanashindwa kumzuia nchini kwakuwa yeye ndiyo mwenye dola hivyo wanatafuta soft target kumhujumu.

wacha kupotosha huoni deni la taifa linavyokuwa then unajifanya hujuhi hela zinatoka wapi?
 
..hapa Tanzania napo wanasiasa wameanza kuhutubia Kikabila.

Inasikitisha sana hii hali mpya maana ukiwepo au kufuatilia safari za Mh. watanzania wengi tunabakia kapa bila kuelewa Rais anaongea nini ktk safari hizi za kikazi zinazogharamiwa kwa kodi za watanzania wote lakini anaongea kilugha na kupelekea kubagua watanzania ktk safari za kikazi.

Kikubwa siyo gharama za kodi za wananchi bali gharama kubwa zaidi ni kubomoa umoja na utaifa wa nchi hii mama Tanzania halafu Prof. Kabudi anawadanganya waKenya kuwa waTanzania hasa viongozi wa awamu hii 'hawakuzi' makabila na ukabila.
 
bagamoyo,

..ukiacha hilo la kuzungumza KILUGHA, Prof amekuwa bingwa wa kuhuburi ZABURI ktk shughuli za KISERIKALI.

..badala ya kuwaelekeza wateuliwa ktk nafasi mbalimbali wakasome na kuzingatia sheria, katiba,na miongozo, Prof amekuwa akiweka msisitizo ktk ZABURI.

..mambo haya yananifanya nijiulize, Je Waziri Jaffo naye anapaswa kuanza kutoa mihadhara na kunukuu KORAN tukufu ktk shughuli za serikali? Je, atavumiliwa au atashambuliwa kuwa ni mdini?
 
Bonge ya speech dadeki....
sema wabongo tunamchukulia poa sana huyu jamaa.....
ubongo wake ni mpana sana...
 
wacha kupotosha huoni deni la taifa linavyokuwa then unajifanya hujuhi hela zinatoka wapi?
Kukopa kweli tunakopa lakini kuanzia 2016 mpaka 2019 takwimu zinaonesha deni limeongezeka kutoka 36.4% mpaka 37.7% ya GDP. Hili ni ongezeko la 1.3% ya GDP.

GDP(nominal) yetu ni $61b na ongezeko la 1.3% ni sawa na $793,000,000 (trilioni 1.82Tsh). Sasa kiasi cha mwanzo tuu kilicholipwa kujenga SGR ni $1.2 billion (trilioni 2.76Tsh) ambayo ni zaidi ya pesa tulizokopa kipindi cha miaka mitatu. Hizo pesa nyingine za kununulia ndege, kujenga bwawa la umeme, barabara, bandari, viwanja vya ndege n.k unafikiri zinatoka wapi?

Screenshot_2019-11-28 Tanzania - national debt in relation to gross domestic product (GDP) 202...png


 
Back
Top Bottom