WAZIRI WA MAMBO YA NJE TANZANIA PROFESA PALAMAGAMBA KABUDI AWAJIBU MABEBERU, HATUJAWAHI KUPIGISHWA MAGOTI, UCHAGUZI ULIKUWA HURU NA HAKI
Waziri wa Mambo ya Nje Prof. Palamagamba Kabudi aijibu EU - Umoja wa Ulaya kufuatia kikao cha bunge hilo la ulaya huko makao makuu ya EU kutishia uwezekano wa vikwazo kupitia Kamati yake Mambo ya Nje ya Bunge la Umoja wa Ulaya kujadili uwezekano wa kuibana Tanzania kwa vikwazo vya aina mbalimbali ikiwemo kusitisha msaada wa kuifadhili bajeti ya Maendeleo ya Tanzania.
Prof. Palamagamba Kabudi ameomba msaada wa vyombo vya habari nchini kuisaidia serikali ya Tanzania kwa kujitokeza na kuieleza Jumuiya ya Kimataifa ukweli wa mambo. Na kueleza Nyerere aliwahi kuwadindia Germany na United Kingdom na kukataa misaada na fedha zao. Prof. Palamagamba Kabudi anashangaa waTanzania kuanza kutetemeka ktk mitandao ya kijamaii kuhusu nchi yetu kuwekewa vikwazo.
Prof. Palamagamba Kabudi amesema Tanzania haifuati sera za kidiplomasia za kujitenga kufanya kazi na Jumuiya za Kimataifa. Hivyo waziri Prof. Kabudi amesema Tanzania ipo tayari kukaa ktk meza moja na wadau wa kimataifa kuzungumzia mapungufu yaliyopo lakini si kwa kuburuzwa na mabeberu bila kuwa na facts mezani.
Prof. Palamagamba Kabudi amesema kuwa watu wahuni wachache wa Kamati ya Mambo ya Nje ya Bunge la Ulaya EU hawawezi kuitisha na kuidhalilisha Tanzania na watambue Tanzania ni nchi huru.
Prof. Palamagamba Kabudi amesema maneno hayo mazito akiongea na Wafanyakazi wa Wizara hiyo muhimu ya Mambo ya Nje akatumia fursa hiyo kujibu uvumi kuwa Tanzania itanyimwa misaada na kuwakumbusha wafanyakazi hao kutembea vifua mbele kwani Tanzania siyo nchi ndogo kidiplomasia, kimsimamo, kiji-Geopolitiki na kiushawishi kimataifa.
.....................................................EU Parliament Committee on Foreign Affairs discussion on Tanzania
Tujikumbushe walioitwa "wahuni wachache" na Prof. Kabudi, tarehe 19 November 2020 jijini Brussels kwa dakika 45 mfululizo walisema nini kuhusu Tanzania ktk kikao cha Kamati ya Mambo ya Nje cha Bunge la Jumuiya ya EUTazama / sikiliza dakika 45 za mjadala ktk kamati hiyo: