Aliyoainisha Mhe Palamagamba Kabudi ni sahihi kabisa kwa upande mmoja wa sarafu lkn kwa mwenye akili aweza kuchambua hotuba ktk maeneo kadhaa kama ifuatavyo:-
(i). Kuhusu Mwl Nyerere kurudisha fedha kwa Uingereza na Ujerumani miaka ya 60 ilikuwa sawa - sasa kwa miaka hii ya 2020 ni sahihi kurudisha fedha sababu ya kulalamikiwa juu ya uchaguzi kughubikwa na mauaji, kutesa, na kukamata wapinzani?
Sawa ameeleza kuwa duniani kote huwa hakuna uchaguzi huru wala haki kwa standards ya 100 lkn amejiuliza kwa nini katiba ilitungwa, amejiuliza kwa nini Sheria zilitungwa? - Ni kwamba viwe vipimo vyetu ktk utendaji wa kila siku;
(ii). Madai ya kero za uchaguzi (kabla, wakati na baada ya uchaguzi). Hivi tumefika hatua ya kubariki mauaji, unyanyaswaji na ukandamizaji wa kidemokrasia kiasi cha kutambia dunia! Mie nilidhani kwamba angeeleza umma kuwa mambo yaliyojitokeza kwenye uchaguzi yanaendelea kushughulikiwa na mamlaka za ndani na kuahidi kupata suluhu kwa njia za mazungumzo na makundi yanayovutana - sasa chukulia mfano fedha za misaada zizuiliwe - hivi tutakuwa ni ukoo wa binadamu gani?
(iii). Viongozi, ndio wenye maslahi makubwa ya kitaifa sasa wasitengene njia za kuikosesha nchi misaada sababu bado tunaihitaji dunia, bado tuna changamoto kwenye afya, elimu, maji, kilimo, usafiri na usafirishaji, huduma za kiuchumi nk nk - kama tunatofautiana nao tutofautiane kwa sababu zenye uzito kama kukataa ushoga, udini, ukabila au ukanda lkn sababyinayotufanya leo tukosane ni ya kitoto na tunatakiwa kuizuia.
Mhe Palamagamba Kabudi, liangalie taifa hili limejaa watu wenye uhitaji sasa maslahi ya kisiasa kwa kundi dogo si sawa - wanaoathiriwa na kuzuiliwa fedha ni CCM, CDM, ACT, CUF, NCCR na vyama vingine pamoja na wasiokuwa na chama - ninyi mmeapa kutumikia hawa hawa ambao mnataka kuwasitishia misaada - NOT Good at all!
Msakila M Kabende
Kigoma