Prof. Kabudi apologise or resign for embarrassing the president and the country

Yule mzee alidhani hatujui kiingereza.
Tafsiri ya alichoongea thornton na kiswahili alichokuja kupiga yeye ni vitu viwili tofauti vinavyoelekea upande mmoja.

Tumedharauliwa sana!!
Yaani kuambiwa jamaa wanapunguza deni kumbe wao wanaongelea good will ya kutaka kujenga uaminifu
 
Amewekwa kichwa zaidi ya Muhongo kusimamia madini. Maana alishasema huwa hachagui kilaza.
Duh! mh! .Ngoja tutamsikia atakapotoa speech kwa mara ya kwanza tangu ateuliwe.Muda utaamua
 
Na paka shume jerry muro nae sijui afanyaje maana jana alivochonga domo ila huyu Kabudi nae jana alijua kutupa machicha looo halafu aliongea kwa maconfidence si ya nchi hii kumbe chaka
 
Nawaza tu, kama haya yalijulikana kwamba subject to approval kule juu sasa kulikuwa na haja gani ya kupiga mayowe? why tusingesubiri approval au la? hivi sasa tumeleta taharuki kadhaa kwa wenye kuwazia Noah nk.
 
Ukishaambiwa tutakupa kiasi flani in "good will", usishangae kesho yake kuambiwa "aisee mambo yaliingiliana buaanaa". Ile "ahadi" ya USD 300M haikuwa part ya ile invoice hewa ya TRA. Harafu kwenye hiyo statement ya Prof. Kabudi, hakusema chochote kuhusu ile invoice wala hatma ya Makinikia
 
Imefikia hatua hata jerry murro anajiona anafaa kuwa mtetezi wa awamu hii
Uteuzi ataupata tu maana kajifaragua vya kutosha ila anakurupuka sana mithili ya swala asikiapo mvumo wa upepo ukitikisa unyasi
 
Nyinyi watu mliokosa uzalendo, nyinyi watu vibaraka msiojulikana hats kwa mnao wakuadia mtaiombea nchi maovu mpaka link?!!

Mtafaidika nini nchi ikipata madhara?

Acheni ujinga mnaboa?! Huo ni uchawi kabisa.

Hivi hao Accacia walisema hawawezi kulipa? Hawatalipa? Ama hawana fedha za kulipa?

Na kama mdaiwa amesema hana fedha za kulipa, maana yake hadaiwi ama anatambua kuwa anadaiwa lakini hana uwezo wa kulipa?

Kwani Accacia ni nani? Mnafahamu kuwa ndani ya Accacia Barrick ndiye mwenye hisa nyingi 64% na ndiye aliyeingia mikataba na nchi, na ndiye aliyeongoza mazungumzo na serikali.

Kama Barrick wameridhia hayo makubaliano, kwanini nyinyi vibaraka mnashadadia ovyo kauli ya the so called Accacia.

Tumieni akili siyo kuwaza kutumia maeneo mengine. Hii ni nchi yetu sote, ikidaiwa tunaumia wote, ni kodi zetu. Ikiibiwa tunaibiwa wote, hakuna maendeleo kwenye nchi yatapatikana
 
Wale wanacheza na akili tu. Wanajua wapi pa kupigia bao.Unapewa chansi uingie kingi mwenywe.Ukija kugundua umeishaliwa tayari.Ni CARL PETERS hivihivi.
 
Bora Lissu hajafa, kama atapenda kuongelea mbilingembilinge hii watz tutajua mengi.Tutajua jeuri ya wazungu hawa iko wapi na tutajipanga upya tuwakabili.Hatukubali mpaka kieleweke.Ila sifa za kisiasa ziwekwe pembeni twende pamoja tuwakabili hawa majamaa.Ni wajanja, ukiwabana hapa wanaponyokea kule.Hata wao wanataka ushindi.Chuki za kisiasa ni heri kwao.
 
Jamani mbona hamusubiri mhusika mkuu aliyefanya mazungumzo ajibu kauli ya Accacia? Mbona mna mihemko kiasi hicho. Tumsubiri Baricks atajibu au ku-react vipi.
 
Barrick waki wire hiyo USD 300M, Utasema nini?
 
Tusikurupuke mbona watanzania wenzangu mmekuwa maadui kwa nchi yetu wenyewe, hata sisi tunaochangia bila kujua kinachoendelea sijui tunatoa wapi napata shida sijui ni elimu au ushabiki, Taarifa ni kuwa Serikalibya Tanzania haina mkataba na Acacia, Serikali ina mkataba na Barrick na ndio maana haijaongea na Acacia na ndio maana tulioingia nao mkataba wakaja, kwenye ile kamati inatoka Barrick na haitoki Acacia na pia Serikali inaweza kuwachukulia hatua Acacia , kwani wao hawakushiriki kwenye makubaliano sasa wanawezaje kusema hawalipi nani amewaambia wao ndio wanadaiwa tuwache kuwapotosha Wananchi , mwenye ushahidi kuwa serikali iliingia mkataba na Acacia aulete hapa .
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…