Paschal, unasema Kabudi anakabiliwa na vitu fulani, ila kwangu mim namwona kama mwoga kwenye maamuzi na mtu asiyetaka lawama,,hili kwa taasis hii si zuri maana lazima uwe na maauzi la sivyo watakuamulia wengine na utaumiza watu,
Makonda ni mzuri lakini ujana bado unamsumbua yaani utulivu wa maamuzi, kwa muono wangu huyu hafai, Kigwa nae kama Makonda,badae wanaweza kuja kuwa viongozi wazuri sana lakini kwa hii miaka 5 tu ijayo inaweza kuwa bado, Prof Mbarawa yuko vizuri, Mwinyi, yuko vizuri ingawa amekaa na wizara ambayo si rahisi sana kuonekana mapungufu kijamii,
Kwangu raisi ajaye natamani awe our current PM, Majaliwa Majaliwa, kazi inapigwa vizuri tu na maturity ya kimaongozi ipo,,ametulia mzee wa watu kwenye maamuzi na akisema amemanisha, huu ni upande wa ccm
Kwa wenzetu, upande wa pili baada ya Dr Slaa kuondoka, Lisu anaweza kufaa sana lakini bahati mbaya watu wanaweza tumia tukio lake kama fimbo kwake na wakapenyeza vyao,,yaani mataifa ya nje, Lisu yuko vizuri sana lakini kwa hili anatakiwa kuwa mwangalifu akipata nafasi hiyo kusimamia nchi yake, control ya influence ya nje ya mipaka yetu muhimu, nimeweka hii kwa mfano wa Raulent Kabila, Prof Baregu kwa maturity ya kimaongozi pia anaweza kutufaa sana.
Sent using
Jamii Forums mobile app