Prof. Kabudi: Kwa sasa Wananchi hawatapewa dawa za kukabiliana na Corona kutoka Madagascar, inafanyiwa utafiti kwanza

WATANZANIA NIWAMOJA NA TUMECHAGUA KUNYWA DAWA NAHAKIKA HATOBAKI MTU NYUMA JUU YA UNYWAJI DAWA!!!

CCM DAMUDAMU!!!,CHAMA CHA MAMA &BABA
 
Unaweza kushangaa inawezekanaje profesa kufanya ujinga kama huu ila ni wa kuonea huruma tu kwa sababu kufanya kazi na psychiatric president siyo kazi rahisiView attachment 1444696
Nia na madhumuni ya safari ilikuwa kumletea baba dawa, wengine pigeni mzigo mlipe kodi na October msisahau kulichagua jembe kutoka Chato.
 
Nendeni mkatoe hizo dawa kwa wagonjwa halafu mtuletee mrejesho, huwezi kuanza kufanyia utafiti dawa ambayo imeshatolewa kwa ajili ya matumizi.....mbona hapa hapa nchini kuna baadhi ya watu wamedai wana dawa ya korona, halijatumwa hata guta kwenda kuzichukua na kuzifanyia huo utafiti...
 
Hata dawa toka Ulaya ufanyiwa utafiti zina kemikali gani ndani, na kama ni salama kunywa na haina kemikali za ziada pia ni dawa ya kweli sio sumu.

Hata mitishamba inayokubalika na serikali inafanyiwa utafiti kwanza, utafiti huu sio wa kujua kama dawa inaponyesha, ni kujua usalama wake.
 
Hata dawa toka Ulaya ufanyiwa utafiti zina kemikali gani ndani, na kama ni salama kunywa na haina kemikali za ziada pia ni dawa ya kweli sio sumu. Hata mitishamba inayokubalika na serikali inafanyiwa utafiti kwanza, utafiti huu sio wa kujua kama dawa inaponyesha, ni kujua usalama wake.
 
"Hauwezi kwenda Madagascar kuchukua dawa kwa ajili ya Watanzania Wote na ndege ya Rais,

Mngeniona nimeingia kwenye ndege ya Dreamliner au Airbus ndiyo mngejua nimechukua Mzigo ili Watanzania Wote wanywe" - Waziri Prof. Kabudi
 
Nijuavyo mimi msemaji wa maswala ya tiba na dawa kisekta ni waziri wa afya au Naibu wake wakisaidiwa na wataalamu wa wizara.

Lakini kwa hii dawa mpya ya Covid 19 kutoka Madagascar nimeshangaa kuona msemaji wake mkuu ni Prof Kabudi ambaye ni waziri wa mambo ya nje, hapo ndio ninapoomba maana Ummy Mwalimu yupo na anadunda kama kawa.

Hii imekaaje wadau?

Maendeleo hayana vyama!
 
Halafu utafiti wa kuonyesha inaponyesha anafanya nani? Na hizo dawa zingine hufuatwa na ndege ya rais?!

Huu ni ujinga mtupu. Dawa tunazoletewa hazipimwi ni uongo unatujaza, wewe uko serikali gani?!
 
Nijuavyo mimi msemaji wa maswala ya tiba na dawa kisekta ni waziri wa afya au Naibu wake wakisaidiwa na wataalamu wa wizara...
Mbona hata kwenye mambo yamakinikia ndio alikuwa msemaji??πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚ kifupi jamaa yeye ndio kila kitu mzee wakubagaza!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…