Prof. Kabudi: Kwa sasa Wananchi hawatapewa dawa za kukabiliana na Corona kutoka Madagascar, inafanyiwa utafiti kwanza

Kongole kwa serikali, kangole binafsi kwako waziri Kabudi, kongole pia kwa Watanzania wanaosubiri jibu la WHO kupasisha dawa hii ya kutoka Madagascar.

Serikali mmechukua hatua stahili kutufuatia dawa hiyo, si wamethibitisha inatibu! Na ss ugonjwa si upo na wagonjwa wapo? Sasa serikali isifuate dawa? Hapana Kongole kwako binafsi mh Maghufuli " permasharp" wembe mkali.

Kuchunguza kimaabara kabla ya kutumia!! Hekoooo tunayo maabara thabiti, wenzetu wametuthibitishia , zipo dawa asili kibao za Watanzania zenye kutibu magonjwa mbalimbali ziko foleni kusubiri majibu ya kitaalamu ili kupasishwa kwann hiii isipitie hatua hizo.

Watanzania wanaokebehi na kusubiri majibu ya WHO juu ya dawa hiyo, sasa tumewawahi! Subirini WHO SISI tumechukua dawa na tutatoa majibu haraka kwa faida chanya au hasi kwa Watanzania.

Mh Kabudi kanywa kwa maamuzi yake binafsi na kafafanua kuwa kafanya vile kuonesha shukrani kwa Serikali ya Madagascar.

Mungu Ibariki Tanzania, Mungu Mbariki Mh Rais Maghufuli Mungu Tubariki Watanzania.
 
Hapa kwetu ndio kuna mambo ya ajabu huwezi kuyaona katika ulimwengu wote labda ulimwengu wa Roho.

Dawa anayotuambia kuwa imeletwa karibu tani nzima kama SAMPLE ili ipelekwe maabara kwa uchunguzi ameamua kwa hiari yake bila kulazimishwa na mtu kuinywa chupa nzima.
Huyu sio mwingine bali ni Waziri wa mambo ya Nje, Msomi wa kiwango cha Profesa wa sheria na mshauri wa karibu wa Rais.

Jee hii sio hatari kwa dawa ambayo bado ni sample kuinywa? Na kama kainywa Waziri nini kitazuia wengine kuidokoa kunywa hapo NIMRI ikiwa inasubiri kufanyiwa kazi?
Iwapo itakuwa haifai na inahatarisha Afya lawama tumlaumu nani? Aliyemtuma kwenda Madagascar au yeye mwenyewe kwa kuonja chupa nzima bila ruhusa ya aliyemtuma?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Naibu waziri wa ulinzi unamfsham? Tokea nianze kufuatilia bunge sijawai kuona naibu waziri anawasilisha bajeti badala yake ikitokea waziri kamili anadharua anawaailisha waziri mwingne badala yake. Labda utuambie ni lini ulimuona naibu waziri akisoma mapendekezo ya bajeti ya wizara yeyote.
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sidhani kama atagombea tena labda awe ni kichaa kama Mobutu kwa sababu mpaka vikao vya SADC anavikimbia wakati yeye ndiye mwenyekiti!
Duh huyu Mtu bana Mi nimeshindwa ata kuelewa uwezo wake ,Hivi nilini ameweza kuhojiwa na TV yoyote ile ata kama ni TBC
 
Nijuavyo mimi msemaji wa maswala ya tiba na dawa kisekta ni waziri wa afya au Naibu wake wakisaidiwa na wataalamu wa wizara...


Kwanza lazima ujue maendeleo yana chama.

Pili kuhusu dawa, ni hivi; dawa imetoka nje ya nchi na Kabudi ni waziri wa mambo ya nchi za nje hivyo yeye anahusika sana isitoshe yeye amepata pia kuonja hiyo dawa kuonyesha uhusika wake.

Tatu, Ummy Mwalimu hausiki kwa sababu dawa yenyewe bado haijathibitishwa na WHO, yeye kama waziri wa afya hawezi kuidhinisha au kubariki kitu kisichothibitishwa na WHO ambamo TZ ni member, ------ kama yakitokea madhara kutokana na matumizi ya hiyo dawa hapo Ummy atapona na Kabudi akikamatwa yeye ataruka na kusema; "mimi sikuwa waziri wa afya nilionja dawa kama raia tu." 🤣.

That is my take.
 



Fuatilia unaambiwa Prof. Kabudi aliongoza jopo la wataalamu ambapo baada ya kutua Madagascar jopo hilo na wale wa huko walikaa masaa 4 wakijadili masuala ya kitaalamu.
Tunaweza sema Katika hili ni Mwenyekiti wa jopo.
 
Kwa kawaida any medicine in form of Liquid or Tabs lazima iwe na DOSAGE e.g. 1x1, 1x2, 2x2,2x3 a day etc.
Picha zinaonesha watu wanakunywa kwa glasi kama energy drink....Je, hii dawa ni kama kinywaji? Tunaomba ufafanuzi.
Tumeshindwa kujua ni nini hasa, imebidi tuiite Kikombe cha Madagascar, maana hata kike kikombe cha Samunge kilikuwa na dosage yake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…