Kuna kizazi kitakuja kione kizazi chetu ndio kizazi kilichowahi kuwa na wajinga zaidi katika vipindi vyote vya utawala wa Marais just imagine tunaongozwa na huyu maza.
Mimi nadiriki kusema Tanzania haijawahi kushuhudia wakati ambao akili za raia wao zimelala kama zilivyo wakati huu. Tatizo pia linakuwa kwamba, hawa waliopo sasa hivi bado kuna kundi kubwa lililokuwepo pia wakati wa kupata uhuru; na baadhi yao bado ni washiriki wakubwa katika kukilaza akili kizazi hiki cha sasa!
Akina Kikwete, Kabudi; akina Anna Makinda, akina Msekwa; na wengi wengine, ndio washiriki wakuu katika kulaza akili za waTanzania. Sasa tunauliza, imekuwaje hii?
Umegusia "wakuu wa JF"; bila shaka ukiwa na maana ya wachangiaji wa mijadala humu. Unaangalia mijadala yenyewe na waanzilishi wake, imebaki tu kuwa ni mahali pa kufanya uchawa kwa viongozi wanao wapa maslahi.
Nenda kwenye vyombo vya habari, magazeti na hata redio na TV; hali ni ileile.
Siyo kazi ngumu ukitaka kulinganisha. Tafuta tu Daily News, ya akina Philip Ochieng na wengine wa wakati ule; na linganisha na makala hizi katika gazeti lolote lile unaloweza kulisoma leo hii.
Hapa JF pamekuwa sasa ni mahala pa kuleta taarifa za kuonyesha ubovu wa viongozi walio pita kana kwamba wanashindana na hawa wa leo au wa jana; bila ya kujali mazingira yaliyo tofauti kabisa
Na hata hizo taarifa zinazo letwa ni za kutunga tu, kama ilivyo hii hapa inayo mhusu Edward Sokoine, ambaye utendaji wake ulimkosha sana Mwalimu Nyerere.
Kwa hiyo, kizazi hiki cha leo, sidhani kuwa nchi hii itadidimia zaidi ya hapa ilipo fikia sasa hivi. Hapa tulipo sasa ndipo patakapo kuja kuleta mabadiliko makubwa zaidi. Hatuwezi kudidimia chini zaidi ya hapa!