Prof Kabudi: Mwandishi mmoja wa kigeni aliandika kuhusu kifo cha Sokoine kwamba Nyerere alihusika au alifaidika na kifo hicho

..nazungumzia wakati wa harakati za kudai uhuru, na mara baada ya uhuru kupatikana.

..Rashidi Kawawa alijiunga na Tanu akitokea ktk jumuiya za vyama vya wafanyakazi.
haya nayajuwa mkuu.
Wakati wa kifo cha Sokoine, Kawawa hakuwa na 'base' yoyote kwa wafanya kazi au kwinge kokote mbali na CCM. Hata huko CCM kwa kiasi kikubwa alikuwa ni abiria tu.
 
Napata shida sana kumhusisha Rashid Kawawa kwenye mkasa kama huu wa kifo cha Sokoine. Basi tu akili ya binaadam kutunga taarifa na kuieneza ni jambo jepesi sana.
 
Kuna mdau aliwahi kusema wakuu wa JF ni majasiri sana kwenye kujua na kuchambua mambo humu JF ila uraiani hawaonekani nilikuwa sijamuelewa vizuri, ila muda unavyozidi kauli yake naiona iko sawa kabisa.

Kwenye huu uzi wengi wanaona Nyerere hakustahili kuongoza kipindi hicho, wengine wakituhumu aliongoza kizazi cha wajinga meaning hata wazee wenu waliokuwepo enzi hizo walikuwa wajinga pia.

Sasa hapa unajisahau mjinga plus ambaye unaongozwa kipindi hiki chenye kila namna ya kupata taarifa sahihi ila bado wanatuongoza watu wa hovyo na wanagawana mali za umma sie tupo tu hatuna reaction yoyote. Na kuna muda tunatukanwa kabisa kama hataki kulipa kodi hama nchi, mara tuitwe mbwa yaani na hatuna cha kufanya.

Kuna kizazi kitakuja kione kizazi chetu ndio kizazi kilichowahi kuwa na wajinga zaidi katika vipindi vyote vya utawala wa Marais just imagine tunaongozwa na huyu maza.

Then unajikuta mjanja kusema walioongozwa na Nyerere ni wajinga. 🤠🤠
 
Si mgeni lakini sijawahi kuona utapeli wa Kabudi.Infact katika mawaziri ambao nimeshawahi kuwapenda,Kabudi ni mmoja wapo.Ni mwamba aliye na misimo isiyotumba na mizuri.Tanzania tunahitaji viongozi aina ya Kabudi.
Pro Kabudi huyu huyu alieokotwa jalalani.
 
Dumisani Dube alishafariki na kuzikwa South Africa
 
Siku hiyo nilikuwa natafuna hamburger tukiwa na Mkenya mmoja pale Metropole,Arusha akasisitiza bila ushahidi kuwa haya ni mauji kama ya Tom Mboya huko kwao.
Juhudi zangu zote za kukanusha zilishia kwenye masikio ya Chura Kiziwi.
Thom Mboya alifariki mwaka gani kweli?
 
Unatolea mifano ya wanajeshi ambao wakati wa mwl wenu walikuwa wanalipwa vimishahara vinavyoishia kwenye ulevi wa pombe ndio maana walitaka kumpindua.
 
Nyerere Kama walivyo intelligent leaders alikuwa surrounded na wasomi wengi wabishi. Survival was very important at the time. Chagua Kambona au Kawawa, obviously Kawawa ndiyo atakusikiliza, watu kama Kambona walikuwa mwiba.

Tafuta historia ya Kawawa soma halafu linganisha na wengine Kama Kambona
 
Kuna kizazi kitakuja kione kizazi chetu ndio kizazi kilichowahi kuwa na wajinga zaidi katika vipindi vyote vya utawala wa Marais just imagine tunaongozwa na huyu maza.
Mimi nadiriki kusema Tanzania haijawahi kushuhudia wakati ambao akili za raia wao zimelala kama zilivyo wakati huu. Tatizo pia linakuwa kwamba, hawa waliopo sasa hivi bado kuna kundi kubwa lililokuwepo pia wakati wa kupata uhuru; na baadhi yao bado ni washiriki wakubwa katika kukilaza akili kizazi hiki cha sasa!

Akina Kikwete, Kabudi; akina Anna Makinda, akina Msekwa; na wengi wengine, ndio washiriki wakuu katika kulaza akili za waTanzania. Sasa tunauliza, imekuwaje hii?

Umegusia "wakuu wa JF"; bila shaka ukiwa na maana ya wachangiaji wa mijadala humu. Unaangalia mijadala yenyewe na waanzilishi wake, imebaki tu kuwa ni mahali pa kufanya uchawa kwa viongozi wanao wapa maslahi.
Nenda kwenye vyombo vya habari, magazeti na hata redio na TV; hali ni ileile.
Siyo kazi ngumu ukitaka kulinganisha. Tafuta tu Daily News, ya akina Philip Ochieng na wengine wa wakati ule; na linganisha na makala hizi katika gazeti lolote lile unaloweza kulisoma leo hii.

Hapa JF pamekuwa sasa ni mahala pa kuleta taarifa za kuonyesha ubovu wa viongozi walio pita kana kwamba wanashindana na hawa wa leo au wa jana; bila ya kujali mazingira yaliyo tofauti kabisa
Na hata hizo taarifa zinazo letwa ni za kutunga tu, kama ilivyo hii hapa inayo mhusu Edward Sokoine, ambaye utendaji wake ulimkosha sana Mwalimu Nyerere.

Kwa hiyo, kizazi hiki cha leo, sidhani kuwa nchi hii itadidimia zaidi ya hapa ilipo fikia sasa hivi. Hapa tulipo sasa ndipo patakapo kuja kuleta mabadiliko makubwa zaidi. Hatuwezi kudidimia chini zaidi ya hapa!
 
Angeongoza ila kwa kuua watu wengi zaidi ya Samia anavyoua sisimizi
hata zamani ameua sana. nashangaa akina Buti sijui Butiku anapata wapi moral authority kusikitishwa na mauaji ya sasa wakati alikua mshirika na mbariki mauaji na mateso zama za awamu ya 1 tena akiwa mmoja wa perpetrators wa ngazi ya juu.
 
hata zamani ameua sana. nashangaa akina Buti sijui Butiku anapata wapi moral authority kusikitishwa na mauaji ya sasa wakati alikua mshirika na mbariki mauaji na mateso zama za awamu ya 1 tena akiwa mmoja wa perpetrators wa ngazi ya juu.
Wataje tu mkuu 'Meru' tupo tayarikabisa kukusikiliza; hao walio uliwa walikuwa ni ndugu zetu pia.
 
Unatolea mifano ya wanajeshi ambao wakati wa mwl wenu walikuwa wanalipwa vimishahara vinavyoishia kwenye ulevi wa pombe ndio maana walitaka kumpindua.
Usijidanganye, thamani ya hivyo vimishahara unavyosema vilikuwa afadhali miaka hiyo baada tu ya mkoloni. Adjust na inflation utashangaa kwa life style ya wakati ule maisha hayakuwa magumu. Kila kitu kiliharibika baada ya vita ya nduli
 
Excellent
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…