PreGE2025 Prof. Kabudi: Nyerere alitabiri ujio wa Rais Samia miaka 81 iliyopita

PreGE2025 Prof. Kabudi: Nyerere alitabiri ujio wa Rais Samia miaka 81 iliyopita

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
5,383
Reaction score
18,776
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Profesa Palamagamba Kabudi amesema umahiri wa uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan unatokana na juhudi zilizofanywa na waasisi wa Taifa la Tanzania katika kuwaandaa viongozi.

Snapinst.app_486069413_18469984678068597_6063325724283970391_n_1080.jpg
Profesa Kabudi ametoa kauli hiyo leo Machi 24, 2025 katika mdahalo wa kongamano la kumpongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutimiza miaka minne ya mafanikio katika kuliongozaTaifa la Tanzania, mdahalo uliofanyika kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC).

Kupata taarifa na matukio yanayojiri kuelekea uchaguzi mkuu kwa kila mkoa ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

"Dkt. Samia Suluhu Hassan ni matunda, zao la urithi wa waasisi wa Taifa letu, Baba wa Taifa Hayati Julius Kambarage Nyerere na Mzee wetu Hayati Sheikh Abeid Amani Karume. Amelelewa, amekuzwa ndani ya Chama cha Afro Shiraz na baadaye ndani ya chama cha CCM,"

"Miaka mingi alikuwa Mjumbe wa Kamati Kuu, kwa hiyo ni mtu ambaye chama kimemlea, kimemkuza na ametoa mchango wake ndani ya chama na sasa anatoa mchango wake katika uongozi wa juu wa Chama cha Mapinduzi lakini na uongozi wa juu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzanzia"
. amesema Profesa Kabudi

 
Hivi duniani kote Huwa wanafanya huu upuuzi wa kusherehekea kukaa madarakani Kwa miaka kadhaa au ni hapa Bongo land,, nchi zilizokosa vipaumbele ni tabu tupu
 
Mtaongea lolote ilimradi mbaki madarakani tu lakini haiwasaidii kitu
Unajua kuna watu wakiongea utumbo ili wabaki madarakani unawaelewa. Wapo wanaume wazima waliofikia hatua hata ya kukata viuno ili kuhifadhi uteuzi wao. Lakini huyu Professor hafanani kabisa na maneno anayoongea kuwapaka mafuta watu wanaomteua. Wapo ma-professor wanaojitambua hapa nchini watakuwa wanamdharau sana kwa hii tabia. Halafu alitoka na First Class ya Sheria sasa.
 
Unajua kuna watu wakiongea utumbo ili wanaki madarakani unawaelewa.Wapo wanaume wazima waliofikia hatua hata ya kukata viuno ili kuhifadhi uteuzi wao.Lakini huyu Professor hafanani kabisa na maneno anayoongea kuwapaka mafuta watu wanaomteua. Wapo ma-professor wanaojitambua hapa nchini watakuwa wanamdharau sana kwa hii tabia. Halafu alitoka na First Class ya Sheria sasa.
Huyu alikuwa na heshima alipokuwa huko chuoni baada ya kuteuliwa akaanza kukengeuka
 
Huyu babu naye eti ni Professor, hivi nani huwa anawapa u-Professor hawa vilaza? macho kama mjusi amebanwa na mlango.
 
Wazanzibar wanatakiwa kumuheshimu na kumuenzi John Okello. Field martial John Okello alikuwa ni mwanachama wa chama cha Afro shiraz party na ndiye aliyewafurumusha waarabu wakakimbia kutoka zanzibar.Field martial John Okello ndiye champion wa mapinduzi ya zanzibar.

Historia ya neno "mapinduzi" inatakiwa kutajwa pamoja jina la field martial John Okello, Mhaya kutoka Mutukula.

Jina la John lina historia kubwa kuhusu uasisi wa Tanzania kuliko jina la samia. Wenye majina ya John kama John Magufuli au John Heche wana affinity kubwa ya uasisi wa taifa hili ndio maana sishangai kuona John Magufuli alifanya makubwa kwa Tanzania na sasa John Heche anafanya makubwa Chadema na Tanzania yote.
 
Back
Top Bottom