Prof. Kabudi: Rais wa Ufaransa amwandikia Barua kumpongeza Rais Magufuli kwa kuiwezesha Tanzania kuingia Uchumi wa Kati

Prof. Kabudi: Rais wa Ufaransa amwandikia Barua kumpongeza Rais Magufuli kwa kuiwezesha Tanzania kuingia Uchumi wa Kati

Mambo haya hayahitaji hasira ni ya kidiplomasia zaidi

Wanamitandao kuweni na utulivu mliyoyatarajia huenda yasitokee kabisa.

HAPA KAZI TU
Yule kiwadi alienda huko analalamika ati warembo wetu.marafiki zetu hawakubali kuiwekea vikwazo Tanzania kwa kuwa ni.stable ,mwanasheria hajui issue zinazo mount kuingia ICC .mwisho wa aibu tupu
 
Ningefurahi kama kabudi kwa sasa angetumia weledi wake wote kuweka mambo yote sawa awafuate mabeberu akae nao awaeleze jinsi uchaguzi ulivyoenda wamuelewe waachie shekeli
 
Rais wa Ufaransa Emanuel Macron amuandikia Barua kumpongeza Rais Magufuli kwa kuiwezesha Tanzania kuingia Uchumi wa kati miaka mitano kabla ya muda uliopangwa

Serikali imesema katika kipindi cha pili cha awamu ya pili ya uongozi wa Rais wa Jamhuri ya Muuungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli itajikita zaidi katika kuboresha uwekezaji wa ndani na nje ya nchi na kuimarisha ushiriki wa sekta binafsi katika kujenga uchumi wa nchi

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi ameyasema hayo wakati alipokutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Ufaransa hapa Nchini na kuongeza kuwa baada ya kipindi cha kwanza cha miaka mitano ya uongozi wa Rais Dkt John Pombe Magufuli kujikita katika uwekezaji mkubwa wa maeneo ya miundombinu na nishati pamoja na huduma za kijamii sasa serikali inalenga kuimarisha ushiriki wa sekta binafsi katika ujenzi wa uchumi.

Balozi wa Ufaransa hapa Nchini Mhe. Frederic Clavier amemkabidhi Prof Kabudi barua ya iliyoandikwa na Rais wa Ufaransa Mhe Emmanuel Macron kwenda kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli kumpongeza kwa kuiwezesha Tanzania kuingia katika uchumi wa kati ikiwa ni miaka mitano kabla ya muda uliopangwa.

Hahahaaaa mimi napita tu humu sichangii.
 
Non-sense. Huyo Kabudi ndio mstari wa mbele kuwaita MABEBERU, leo eti barua, SO what?. Huo uchumi wa kati ni vzr serikali ya jiwe ikasaidia kuelimiasha wanaichi tulipo kuwa uchumi wa chini eg umeme unit moja ilikuwa Tsh 300 na sasa tuko wa kati unit moja TSh 150, lakini huo uchumi wa kati wa kwenye makaratasi, HELL!
Leo kwao ndiyo story kubwa utafikiri shida za wananchi zimeisha
 
Back
Top Bottom