Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 5,383
- 18,776
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Prof. Palamagamba Kabudi, amesema kuwa Serikali haiwezi kuingilia mzozo wa klabu za Simba na Yanga kutokana na kanuni za Shirikisho la Soka Duniani (FIFA), ambazo zinakataza serikali kuingilia masuala ya mpira wa miguu
Prof. Kabudi ametoa kauli hiyo bungeni jijini Dodoma, wakati akihitimisha hoja ya makadirio ya mapato na matumizi ya bajeti ya wizara yake.
Amesisitiza kuwa Serikali itaendelea kushirikiana na wadau mbalimbali katika juhudi za kuboresha mchezo wa soka nchini, na mazungumzo baina ya klabu hizo yalikuwa ni katika kuhakikisha maendeleo ya michezo.