Prof. Kabudi: Tanzania ndio tunaratibu mapambano ya Corona kwa nchi za SADC na Waziri Ummy aliongoza kikao cha kupanga mikakati mwezi Machi

johnthebaptist

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2014
Posts
97,869
Reaction score
171,716
Akiwasilisha hotuba ya makadirio ya wizara ya mambo ya nje na ushirikiano wa Afrika mashariki Prof Kabudi amesema Tanzania ndio mratibu wa mipango ya kudhibiti Corona kwa nchi za SADC.

Prof Kabudi amesema mwezi March mwaka huu waziri wa afya mh Ummy Mwalimu aliongoza kikao cha mawaziri wa afya kwa nchi za SADC na kuweka mpango kazi ambao baadae uliridhiwa na kikao cha baraza la mawaziri wa SADC alichokiongoza yeye ( Prof Kabudi)

Pia Kabudi amesema hivi karibuni Rais Magufuli ambaye ndiye mwenyekiti wa SADC ameziomba taasisi za fedha duniani na nchi wahisani kuziondolea madeni nchi za SADC ili ziwexe kushiriki kikamilifu katika kulidhibiti janga hili hatari la Corona.

Chanzo: Channel ten

Maendeleo hayana vyama!
 
Kwa mambo yanavyoenda hapa nchini, ya kufichaficha taarifa, kamwe siwezi amini taarifa yoyote ya serikali. So hata huyu Kabudi simwamini kabisa.
Ramaphosa na kiherehere chake kumbe alikuwa anaropoka tu

Ramaphosa alishindwa kuwatetea Wananchi wake waliouawa migodini akawatetea Wazungu

Ndio nikijua hamna kitu pale

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hahaha haturatibu chochote, tunalala na kuamka chato tunasikia milio ya ndege asubuhi tunaangalia tv na kupokea simu mbili tatu alafu tunarudi kulala.

Ye anaongelea kikao cha mwezi wa tatu bila hata aibu wakati huo corona haijafika hata Afrika, vijimaneno walivyosema kipindi kile ambavyo hawajakaa kukamilisha ndiyo wanakuja kusema wanaratibu? Nini my ass? Huyu profesa anahisi kila mtu ni mwanafunzi wake kilaza, hayupo serious kabisa, ile dawa ya madagascar imemchanganya akili.

Na ile casual talk ya jiwe kuomba msamaha wa fedha ndiyo anaona kama tunaongoza vile kwenye kupambana na covid? Hahaha ile nayo ataita effort? Hela wamewapa Kenya na Rwanda, sisi tufanyeje sasa? Tukae tujifukize? Nyambaf
 
Hapana hapo maendeleo yana vyama

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Muongo huyu Magamba Kabudi. Magufuli anatafutwa anasema waandike yale yote yatakayozungumzwa. Muulizeni Magufuli ana kimbia nini? Mbona anawakimbia wenzake?
 
Mratibu co-ordinator aliyeshindwa kujenga ushawishi na imani kwa SADC na halafu kisha anafungiwa mipaka wacha ajigambe Dodoma lakini huko Rusumo, Tunduma, Namanga, Horohoro, Mutukula waTanzania wanabaki kushangaa kama kweli Tanzania ina ushawishi.

Membe atema cheche: Tanzania tunatengwa na majirani zetu, wanahisi tunasambaza Corona nchini kwao

 
Pia Kabudi amesema hivi karibuni Rais Magufuli ambaye ndiye mwenyekiti wa SADC ameziomba taasisi za fedha duniani na nchi wahisani kuziondolea madeni nchi za SADC ili ziweze kushiriki kikamilifu katika kulidhibiti janga hili hatari la Corona.
Wananchi wengi wanatamani kuona print out as official statement ya SADC kuhusiana na janga hili. We need to come out as a major block in Sub-Saharan Africa kudai debt relief along with other initiatives to curb the impact of coronavirus to our economy
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…