Prof. Kitila: CCM haiwezi kufundishwa demokrasia na yeyote nchini

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
5,383
Reaction score
18,776
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais- Mipango na Uwekezaji, Prof. Kitila Mkumbo, ametoa jibu kali la kiitikadi dhidi ya vyama vya upinzani vinavyoishutumu serikali kwa kubana demokrasia, akisisitiza kuwa chama tawala cha CCM kina historia ndefu ya kupigania haki na kiko imara kisheria kufuatia ushindi wa Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025.

Akihitimisha hoja na kulitaka Bunge kupitisha Hali ya Uchumi wa Taifa kwa Mwaka 2025 na Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa Mwaka wa Fedha 2026/2027 leo Jumanne, Juni 23, 2026, Prof. Kitila ametumia vifungu vya Katiba ya CCM na Ilani ya Uchaguzi kuondoa dhana inayojengwa mtaani na majukwaani na viongozi wa upinzani akionesha kuwa misingi ya utawala bora imelindwa kimfumo.

Soma: Prof. Kitila Mkumbo: Tanzania haitakubali kupangiwa marafiki wala maadui

Ameanika takwimu za kiutawala akibainisha kuwa neno "Haki" limetajwa mara 32 ndani ya Katiba ya CCM ya mwaka 1977, jambo linalothibitisha kuwa demokrasia ni DNA ya chama hicho tangu asili yake kinadharia na kimatendo.

Amesema chama kinaamini kuwa misingi imara ya utawala bora, haki za binadamu na utawala wa sheria ni nguzo muhimu zinazohakikisha Tanzania inaendelea kubaki na amani na utulivu wa kiuchumi kwa ajili ya kuvutia uwekezaji.

Huyu msegejuakali njaa achana naye
 
Wakati wa DP WORLD MKUMBO,WASIRA Ndio walitumwa na CCM kusambaza propaganda za kishetani
 
Back
Top Bottom